Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KASHESHE🤣 kiswahili ni kazi sana Mungu akasaidie wanao utakao wazaa.Nmesoma nusu nmeona umeandika utumbo kwa kweli. Hiyo sio sabab kabisa. Ttizo kibonzo umekikuta sehem na ww ume copy kama ulivosema em fanya utaft wa kwako alaf ulete hapa.
What a https://jamii.app/JFUserGuide?Habari ya asubuhi.
Nimekutana na hiki kibonzo mtandaoni nikasema acha ni share
Wanaume wengi sasa wanalalamika wanawake wamekua na elements za u-masculine au wanaonesha ungangari lakini mnajua sababu?
Unakuta mwanaume yupo ndani na mkewe,
Bulb imeungua usiku mwanaume anasema anampigia fundi kwa simu hapatikani so wanalala giza. Bro hawezi kubadilisha bulb.
Wanatembea na gari inapata pancha mwanaume anashika kichwa hajui anafanyaje anamtafuta fundi abduli wa magari hampati safari inaishia hapo.
Najua mtabisha lakini nawaambia masculine men wapo wachache sana sana sana sana na hiko ndo kinawafanya wanawake wavue gamba la unyonge waanze wao kujaribu kufanya hivyo vitu ili gurudumu liende. Wakishajaribu tayari wanaume wanakasirika wanakwambia mwanamke anataka kushindana na nature,
Mwanamke anataka kujifananisha na mwanaume. Nani kakwambia wanataka kuwa kama nyinyi?
Mnafika sehemu unakuta mhuni anamkosea heshima mwanamke mbele ya mwanaume wake, mwanaume anashindwa kustep up kwa ajili ya mwanamke wake, anakaa pembeni anasema ye hapendi shari. Hivi hapo huyo mwanamke atafanyaje kama sio kujivika vazi la umasculine na mara nyingi changamoto zinaanziaga hapo.
Wanawake wanajipambania kwasababu mwanaume waliemkabidhi nafasi ya uongozi anashindwa kukaa kwenye nafasi so mwanamke ana feel hayuko protected,
Kila mmoja ana nafasi yake katika uhalisia lakini mmoja anaposhindwa kuisimamia nafasi yake automatically huyu mwanamke itabidi aanze kujipambania mwenyewe. Sijasema hizo ndo sababu pekee zinazofanya mwanamke aone she has to step up zipo nyingi sana na hii kitu haiibuki tu out of nowhere unakuta ni kitu kimejijenga.
Ngoja niwape mfano, mtoto wa kiume analelewa zile familia za ‘daddy I’m going’ kila kitu anafanyiwa, nguo anafua dada wa kazi hadi akifika chuo, hata nyasi zikiota nyumbani anaitwa kijana wa jirani au houseboy anafanya. Huyu mtu akipata familia yake af ye ndo awe baba lazima utaskia malalamiko na kwa bahati mbaya akikutana na mwanamke wa opposite yake lazima watagombana kwasababu mwanamke anategemea Baba atafanya, baba hafanyi, mwanamke anashika kifaa anajaribu kufanya mwenyewe-tayari anataka kushindana na mwanaume.
Haya unakuta sasa ndo hizi familia zetu za kawaida, kijana amemaliza chuo anategemea kuna kazi za 9-5 atakaa ofisini anajishkiza sehemu kwenye ofisi anatafuta na mke anaoa, bahati mbaya akipoteza ile kazi ndo basi anarudi nyumbani anashinda na playstation ( najua mtabisha lakini hawa watu wapo) wengine wanashinda kwenye simu tu lets say ni kwasababu ya frustration hivi hapo nani atabidi a step up!!
Ili familia iende itabidi yule mwanamke asimame akapambane familia ile na watoto waende shule.
Haya huu ni ukweli ambao wengi hamuutaki, wanaume wengi sasa hivi hawataki wanawake ambao hawana kazi. ‘Utaskia pambana mamie tusaidiane majukumu.’ Seriously. Sasa unakuta wanaume wengine nje wanadhani yule mwanamke ni feminist sijui anataka 50/50 hawajui ndani ya nyumba anaishi na mwanaume wa aina gani. Unakuta mwanaume anasema kabisa mimi nta deal na ada na kodi ya nyumba wewe deal na kulisha familia, mifano hai ipo kabisa. Hawa wanawake ndo mnaokutana nao humo makazini hawana furaha maana nyumbani hakuna furaha, mume hana muda nae wote wana stress za kazini, inabidi a meet end needs za kuprovide part yake. Two bulls in the house🤦🏾♀️
My call is for some men to step up.
Protect your ladies, stand up for your families, let your woman know that she has a man inside. Hata kama hujui kutengeneza gari amka asubuhi fungua bonnet shika shika hata betri pale gonga gonga hata kachuma kamoja, shika hata wheel spana kaza tairi yani kuwa busy uone mwanamke anavyo feel.
Wanaume nilikua nasubiri sana zitokee mada za kusema ukweli wa kwanini hali sasa imebadilika naona mnatupia lawama kwenye end result tu hamsemi chimbuko la tatizo. Baadhi yenu mmekulia kwenye maisha tofauti sana so kila mtu ananamna yake ya kuendesha majukumu ya familia yake. Yaani mwanamke anaona bila kupambana hapa watoto wangu hawatasoma. Mwanaume kila akija anasema hajalipwa mshahara of which kwa wengine huwa ni kweli kwa wengine ni njia ya kukwepa majukumu. Nini kitatokea?
I call out for peace humu. Sitegemei heka heka zozote wala nadharia za hawa watoto wa kizazi hiki. Kama huna any positive comment kindly pita tu.
Kwa wanaume ambao wana project masculine energy kudos to you. Hamjui tu ni kiasi gani mwanamke anashuka na kuuvaa ukike mnapo step up. Having a person you can rely on ni nzuri kwa afya zetu🤝
View attachment 3007949
So right, unajua kuwa na perspectives kama zako kwa wanawake wengi ni ngumu sana kuwa nazo unless awe amesoma na ana emotiona maturity! Ila ukweli unafaa sana I wish kungekua na wanawake wa namna hii wengi, and facts you can't be the second bull lol 😂, kuna parts ambazo kila part inapaswa kuplay. At the same time mm naona mutual partnership ni kitu nadra sana kukipata maana watu wamevurugwa hata wewe pia umesema swala la bills linakuumiza which is wrong! Kama una nafasi, Ila yote kwa yote mwanaume anapaswa kustep up mwanamke anapaswa pia kustep up kwenye ku nurture na kutunza familia.Asante Bro. Japo mimi ni KE.
Huu uzi hauwezi kutembea kwasababu ni ukweli ambao wanaume wengi hawataki kuusema wala kuusikia. wanapenda ku attack wanawake wanaofanya kazi kuwaita feminists na kwamba wanashindana na wanaume. Huwa inanichemsha wakati ukweli upo wazi kabisa.
Nimejaribu tu kuainisha baadhi ya sababu nnazoziona najua wanawake Wengine nao wameona experience kwengine.
Sisi ndo wa kuirudisha nature. Personally mwanaume akinitamkia anataka tugawane majukumu 50/50 namuona ana shida. Let it be automatic I can’t be the second bull in the house. Obviously kuna vitu mwanamke kama anauwezo atafanya tu kama kupamba nyumba, kuhakikisha jiko na vitu viko on point, wageni wakija wakute nyumba safi na chakula kimeandaliwa kwenye mandhari safi yani hivi vyote mwanaume hajui gharama yake lakini ukikuta mwanamke ana kazi yake, ananunua vyombo vya bei mbaya ili wageni wako wakija wapewe chakula kwenye mazingira safi na hata mume anajiskia vizuri. Mfano, mimi mr hajui hata bei ya sahani wala glass za kimjini. alizonunua yeye zile za 3000 moja anaona zinatosha mimi napenda kitu tofauti na nikajua mwanaume anaetunza familia ukimwambia akuletee set ya elegant glass wanauza decanter na glass zake hadi 180,000 lazima mpopoane. Mi sioni ubahili kununua hivyo because it’s my house and I want it classy. Kuna hotpot za laki sita ukimwambia bro anunue anaweza kukupasua😂 mi naelewa kwanini nazitaka hizo wakija ndugu zake ndo nawawekea humo wanamsifia hadi bichwa linataka kupasuka😂 sasa ela yangu hapo hata haiumi kutoa ila ukiniambia tu nilipe bills naona kama unataka unitoe kwenye umama niwe baba lazima pavurugike amani😂 labda awe amekwama na kwa kuwa najua kipato chake wala hatusumbuani. Wanangu wakipendeza na nyumba ikiwaka roho yangu inatulia. Samahani nimekupa mfano wa kike sana ila nilitaka uone ka reality flani.
It’s the little things yani majukumu yanajigawa automatically hata iweje no one can change familia kuwa into 50/50. Wanaume wanatakiwa waturuhusu tuwe In our feminine era. I hope they get to see the point. 🤝
Hiyo pia nimeitolea mfano maana comment yako imemhusisha mwanaume na nguvu moja kwa moja.Mkuu acha kuwa ignorant! Sijasema ndo kipimo nimetolea mfano tu kuonesha jinsi mambo yalivyo!
Asante mkuu🤝What a JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala
Naunga hoja kwa mikono miwili na miguu pia
Asante sana mkuu.So right, unajua kuwa na perspectives kama zako kwa wanawake wengi ni ngumu sana kuwa nazo unless awe amesoma na ana emotiona maturity! Ila ukweli unafaa sana I wish kungekua na wanawake wa namna hii wengi, and facts you can't be the second bull lol 😂, kuna parts ambazo kila part inapaswa kuplay. At the same time mm naona mutual partnership ni kitu nadra sana kukipata maana watu wamevurugwa hata wewe pia umesema swala la bills linakuumiza which is wrong! Kama una nafasi, Ila yote kwa yote mwanaume anapaswa kustep up mwanamke anapaswa pia kustep up kwenye ku nurture na kutunza familia.
Umeongea jambo zuri sana yaan hadi nimekupenda madam
Kiukweli wanawake wameumbwa kutunzwa na kulelewa hii kuwapa majukumu ya familia ni basi tu,,,lkn wanawake ni watu wa kuhudumiwa huo ndio ukweli
Watafanya majukumu lakini kwa shingo upande na wanaweza kuonekana wapo okay na hilo lkn deep down wanaumia sana kwasababu it's not their nature
Walau basi wajitolee wenyewe kufanya hivyo kwa mapenzi yao lkn sio umpangie kwamba this time utacover moja mbili tatu hapana ni uongo
Lkn jambo la pili nakubaliana na wewe kabisa kuna malezi ambayo vijana wanalelewa na kuwafanya kuwa walaini sana,yaani hawajui kufua,kufanya kazi ndogo ndogo tangu wakiwa wadogo matokeo yake ukubwani wanashindwa kufanya hata vitu vidogo tu
Binafsi nashukuru tangu udogoni nilikuwa naambiwa nijitume kufanya mambo bila kuambiwa na mzee wangu,,leo hii naweza safisha hata mazingira yanayotuzunguka sio kwangu tu hata karibu na jirani yangu nikiona kuna uchafu kwakuwa nataka mazingira yawe safi
Leo hii kuna mabinti ambao walidekezwa huko udogoni hata kupika hawajui,matokeo yake wanaolewa wanategemea mahouse girl ndio wasimamie show
Kifupi malezi toka udogoni ni jambo zuri mno,wazazi hata kama nyumbani kuna house boy na house girl hakikisha siku moja moja wanao wanafanya kazi ndogo ndogo ili uwajengee msingi bora mbele ya safari
Kwanini isiwe bills, hapo ndo unapofeli sasa! What is with bills that frustrates you? Kama unanafasi lipa that's true companionship sio sasa eti kwa sababu wewe ni mwanamke hupaswi. Nimeanza kuona kumbe na wewe ni walewalle tu kasoro tarehe🤣Asante sana mkuu.
Nashukuru pia kama umeweza kuona all this positively and in a bigger picture.
Na niwe mkweli mimi hakuna kitu kinani frustrate kama kuwa two bulls in the house I will feel weak. Nataka kaka mkuu awe strong haswa. sasa ili niwe chini tunaanza kwenye majukumu😂 niache nifanye yangu kwa nafasi yangu. We fanya yako kwa nafasi yako. that is really my toxic trait nahisi ni weakness labda mniseme mnirekebishe hata kama ntabisha ila ntajua mnanisaidia😂 na wanavyosemaga ela ya mwanamke hawajui inaenda wapi huwa hawakosei ila vitu tunavyofanya huwa havionekani kwasababu havihusiani na kulipa bills, kununua vyakula vya familia au ada. Ila deep down wababa wanatakiwa waelewe we are their supporters big time.
Sio kwamba hatutoi, tunataka iwe automatic na sio mwanaume aiweke kimpangilio kwamba lazima tulipe ada sijui kodi.Kwanini isiwe bills, hapo ndo unapofeli sasa! What is with bills that frustrates you? Kama unanafasi lipa that's true companionship sio sasa eti kwa sababu wewe ni mwanamke hupaswi. Nimeanza kuona kumbe na wewe ni walewalle tu kasoro tarehe🤣
Kubadili bulb ni taaluma au common sense?Nabadili mwenyewe.
Babu yangu alikua anamuita fundi abadili maana hiyo taaluma hakua nayo.
Yeye alikua mkulima, kwenye issue yoyote inayohusiana na kilimo aliifanya mwenyewe.
Umeme, mambo ya maji na ujenzi hayo aliita fundi labda sisi wanae na wajuu tuwe na ujuzi nayo.
Na Yes alikua baba baba kweli.
It depends na situation huwezi nambia unapata mshahara mnono na ninajua kabisa you can afford to do something then usingizie you are a woman. Japo I know it's not fair to push women to do so, ila nitajua if she can afford it or not. Alaf hio statement ya kusema mwanaume akuzidi kila kitu tyr inaonesha umeleta uzi for your own benefits ili ku feed mitazamo yako, mwanaume sio roboti wa kufulfil kila kitu ndo maana akatafta mwenzaSio kwamba hatutoi, tunataka iwe automatic na sio mwanaume aiweke kimpangilio kwamba lazima tulipe ada sijui kodi.
Si ndo tunahofia hiyo 50/50 wanayotafsiri ni feminism wakati sio. Yani inaonekana kama tunachuana. Napenda mwanaume anizidi kila kitu.
Huwezi amini bro. Sisi tunaotoa kidogo kidogo bado ni kubwa haionekani tu.
Okay...You have always been the best. Thank you🤝
Yani inawezekana tunakosea ila ni nature.
Hatufanyi kazi ili tuwakomeshe au vipi. Yani mimi nataka nitoke kazini nikikutana na mboga ya kununua nipitie, nimeona shati zuri kwa ajili ya Baba watoto nichukue. Wanangu wavae vizuri, it’s alot. Niweze kushiriki shughuli za kijamii ili ku maintain social connection ambazo baba mda mwingi anakua hana.
Yani ni ile
Financial freedom tu ndo tunayoitamani. Hatupendi kusumbua wababa kuhusu mahitaji yetu ila tunapenda watuspoil. Wanaume wengi wakielewa hili kutakua na amani sana
Ooh I understand you.It depends na situation huwezi nambia unapata mshahara mnono na ninajua kabisa you can afford to do something then usingizie you are a woman. Japo I know it's not fair to push women to do so, ila nitajua if she can afford it or not. Alaf hio statement ya kusema mwanaume akuzidi kila kitu tyr inaonesha umeleta uzi for your own benefits ili ku feed mitazamo yako, mwanaume sio roboti wa kufulfil kila kitu ndo maana akatafta mwenza
I see it! Ndo maana nikasema I'll know if she can afford, if that's your point upo sahihi kabisa alot of men hawalioni hilo, that's why inabidi kuwe na openness sio mwanaume hajui hela ya mke inaingiaje na inatumikaje vivyo hivyo kwa mwanamke. Ila mimi najua kuna wanawake hawapo hivyo anapata hio laki 6 na bado hela ya mafuta anaomba huo ni ujinga hat mm sikubaliOoh I understand you.
Basi kuna kasehemu kadogo tu tumepishana.
Sio kwamba tusitoe because we are women. No. Tunafanya lakini havionekani kwasababu men’s point of view kwenye responsibilities zime rely kwenye majukumu wanayoyaona, sisi tuna base kwenye vile ambavyo sio rahisi mwanaume kuona mfano ndo hivyo wageni wamekuja na Baba hayupo, kuna vitu wanawake tunafanya wanaume hawajuagi basi tu. Mfano tunanunua mashuka mapya, tunaextend our budgets ili ku accomodate wale wageni hata kama ni wakwe.
We do but men create expectations ambazo huwa zinaleta shida. Nikupe mfano.
Nna rafiki yangu alikua anafanya kazi ya mshahara wa laki saba take home. Mumewe ana mshahara wa almost 3.8m. Na biashara kubwa sana. Mwanaume alimwambia mkewe a deal na kununua vyakula ndani mwezi mzima kwasababu anafanya kazi ili yeye adeal na kulipa ada ya mtoto. So yule dada akawa anatumia 300000 mafuta ya kwenda kazini. 300,000 mahitaji ya nyumbani na kulipa mishahara wafanyakazi wawili. Anafika week ya tatu ya mwezi mshahara wake umeisha akimuomba mwanaume anamuuliza umeufanyia nini mshahara wote ule. You see where the thing comes?
Haka kamstari ka mwisho kame ‘kompliketi’ bro😂 sasa akitafta mwenza ndo atamsaidia kwenye bills? Au atamuongezeaIt depends na situation huwezi nambia unapata mshahara mnono na ninajua kabisa you can afford to do something then usingizie you are a woman. Japo I know it's not fair to push women to do so, ila nitajua if she can afford it or not. Alaf hio statement ya kusema mwanaume akuzidi kila kitu tyr inaonesha umeleta uzi for your own benefits ili ku feed mitazamo yako, mwanaume sio roboti wa kufulfil kila kitu ndo maana akatafta mwenza
Okay we are on the same page. Hiyo mshahara wa laki sita na anaomba ya mafuta si aelezee ameimalizaje haina shida kumwambia mume kwamba nilifanya hiki na hiki nimeishiwa naomba ni boost next time ntajitahidi kubalance budget. I think itakua poa zaidiI see it! Ndo maana nikasema I'll know if she can afford, if that's your point upo sahihi kabisa alot of men hawalioni hilo, that's why inabidi kuwe na openness sio mwanaume hajui hela ya mke inaingiaje na inatumikaje vivyo hivyo kwa mwanamke. Ila mimi najua kuna wanawake hawapo hivyo anapata hio laki 6 na bado hela ya mafuta anaomba huo ni ujinga hat mm sikubali