Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Haya majina yaliyotoka wamechambua akina nani? Maana kuna vituko vingi sana.

Kwa mfano rafiki zangu wana degree za IT ila hawamo kwenye shortlisted ya kwenda kufanya usaili ila mtu cheti cha short course za ICT jina lake limo..
Degree ya IT ndio nini ata watoto wa darasa la tano ukiwapa iyo kazi wanaifanya kwa ufanisi.
 
nakushauri tu si kwa ubaya lakini secure a good job Broh utapata semina za kutosha posho na marupurupu kibao mwaka 2032 zikitangazwa ajira za mda uwaachie vijana walau wakusanye mtaji wa umachinga wewe na elimu yako sio wa kuitwa kwenye usahili na vijana wa form iv form six leavers
 
Ndugu wawili wilaya XYZ mmoja kasoma ualimu na mwingine uhasibu wote wamepata afisa tehama ....[emoji23][emoji23]kifupi hawana hata vyeti vya shoti kozi ya Tehama ila wamepata nbs wametishaaaa mamaeee
Napata shida kuamini kama kweli NBS wamechambua Yale majina ya watu walioomba mtandaoni au walioocha nakala kwa watendaji , MTU kaomba ukarani ila kapangiwa kwenda kufanya usaili wa Tehama.
 
Naomba kujua possible questions zitakazoukizwa kwenye upande wa interview ya I.T maana afisa Tehema aliyechagulowa kwenda kufanya usahili kupitia kata yangu ni mmoja na hayupo. Nataka nikapige usahili nikabe gap ilo. Mwenye possible questions atupe hapa
 
Sielewi,kwani walimu hta wa primary hakuna mwenye degree/master? Hakuna ajuae computer?? Naona mnawananga sn walimu
Afu pia hao fm4 hawakupaswa kupata au?? Ni degree tu ndo wenye sifa??? Kupata au kukosa ni kudra ya mwenyezi mungu,kuwa na CHETI Cha tehama haimaanishi ni mtaalam sn kunizidi mm nisie na hcho kikaratasi..!!
Mwisho,,uliekosa shukuru na uliepata shukuru pia,isingewezekana wooooote mpate HAIWEZEKANI..! Na kwataarifa yenu ,wenye elimu ndg wanaangaliwa sn coz hawana usumbufu na ujuaji km nyinyi wasomi wa miaka hii
 
kuna mahala inabid jobukess tutizamwe hata tutengewe fungu la kutukwamua kwa mikopo isiyo na riba
Mikopo ipo halmashauri kwa vijana (mwisho miaka 35). Ila upatikanaji wake ni kwa mbinde sana. Ingetolewa kama individual loan na siyo kwa vikundi kwani kila kijana ana malengo yake na uwezo wake. Vikundi vingi vimefeli
 
Umeandika Upupu Tuuu,, hao wasomi wanausumbufu gani? yaan Ww unauhakika Kuwa Wasomi ni wasumbufu kuliko Form 4 ebu lete ushahidi hapa....Eti uchukue kilaza aliyepata mswaki wa hesabu akahesabu watu unamuacha Msomi mwenye uelewa mpana zaidii wa hesabu na Technologia...... Alafu unapanua Domo lako kuongea na kuandika hovyo hovyo,,,,,,, Ebu waacheni waliokomaa Na Elimu mkashindwa kuwaajiri Wapate pesa za kujiajirii
 
Samahani wazee kwa mwenye taarifa za majina ya waliochaguliwa nafasi ya ukarani Arusha mjin atupe info, jana moshi naskia washatoa majina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…