Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Nmekutana na Mwalimu wangu wa sekondari kwenye usaili...nilivyoingia tu akanitambua kisha akatabasamu akaniambia "Dogo vipi?" Nikaitia, halafu akaniuliza unanikumbuka nikamjibu "ndiyo"
Akaniambia "ok kila la kheri" nikasepa, interview yangu ikawa imeishia hapo.

Kweli nmeamini kujuana kupo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]subilia majina yatoke ndo usherehekee Mana figisu zipo nyingi
 
Yaani hii dunia kama maneno yangekuwa siraha basi waswahili na kiswahili chao ingekuwa nyuklia
 
Jopo lawatu wanaowafanyia usaili alikuwa yeye peke ake????
 
Mie naenda nikapime upepo aisee.
Nimepigwa za uso, nimefika nikawakabidhi magamba yangu acha waanze kutafuta jina, walikuwa kama sita hivi mie nawacheki tu, wanauliza ka nimeona jina langu kwa mtandao nikawajibu sinauhakika sana sababu najua maelekezo ya NBS ni majina yabandikwe katani na huko kwa ofisi za kata hayapo, kazi nimeomba na nimekuja kwenye interview....wakaangua kicheko, wakasema wamelekezwa wafanyie usaili majina walopewa tu lakini wakanipongeza sana kwa kupambana....[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…