Hili zoezi serikali isipotilia mkazo wa ajira kutolewa pasipo upendeleo zoezi litakuwa gumu maana naona mgomo wa kimya kimya kutohesabiwa.
Watu watasema waliopeana connection basi wajihesab wenyewe na familia zao ama kutoa taarifa ambazo sio sahihi.
Sio jambo la busara kumpa ajira mtu mwenye ajira tayari wakati kuna vijana kibao mtaani wanasota hawana ajira.
Serikali iwe makini na watu iliowaamini kufanya usaili maana wao tayari wamepewa nafasi za upendeleo kuwa wasimamizi wa maudhui pasipo kufanyiwa usaili halafu wao wanataka kuwaonea vijana wasio na connection.