Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Kwa hiyo wale ambao hawakuacha kopi kule katani inakuaje? Ina maana NBS hawatatuma majina Katani?
Mkuu Hiyo Copy Haina Ishu Sanaa.
Labda Kama Mtendaji Ataamua kukaza, na inaweza ikawa ndo Sababu ya kupunguza Watu kwenye Usahili Lakini kama Mtendaji upo nae Vizuri hakuna Tatizo kikubwa jina lako lirudi katani na Mtendaji kula nae sahani moja Basi.
 
Fafanua vzr mkuu,
Kwamba Kata ndiyo watatoa majina kwa nbs badala ya nbs ndiyo wawape majina Kata kwa hoja kuwa ni ili nbs wajiridhishe kuwa muombaji ni mkazi wa eneo husika.

Mkanganyiko wangu ulipo ni kwa nin nbs wawe na mashaka na muombaji kuwa mkaazi wa eneo husika haliyakuwa wakati wa kutuma maombi kuna fomu ilikuwa inajazwa na muombaji,wadhamini wake lakini pia uongozi wa serikali ya mtaa/kijiji kwa maana ya mtendaji wa mtaa.

Swali langu.
Mtendaji wa mtaa/kijiji aliwezaje kumsainia fomu muombaji na ikatumwa nbs bila yeye kujiridhisha kama muombaji ni mkaaji halali wa eneo husika na kama hiyo haitoshi akachukua nakala ya fomu hiyo na kubaki nayo ofisini kwake na sasa hao nbs bado warudi tena kutaka ushahidi wa ukaazi wa muombaji kwenye eneo husika?
 
Hiyo Ni nadharia Mkuu Wala usiwe na presha.
NBS hawawezi na hawana muda wa kuhakiki kuwa huyu MTU ni mkazi wa Kata husika Kwa Namna yoyote ile hasa ukizingatia muda umeenda Sana.
Na ndo maaana ili Zoezi la uhakiki linafanywa Kwa kiasi kikubwa na Watendaji wao ndo kila Kitu.
NBS wao uhakiki wao ni kuangalia zile taarifa ulizotuma ni Sahihi na zinaohana na TAARIFA za Watendaji.
NBS hawana ishu KUBWA hapo
Mchawi Ni Mtendaji Yeye Ndo Kila Kitu.
 
Humu kila mmoja anaongea la kwake hakuna mwenye uhakika, nadhani muda ndio utakao amuwa mbivu ni ipi na mbichi ni ipi?
 
Hivi ulishawahi kushiriki zoezi lolote la Sensa toka uzaliwe?
 
Usiishi kwa kukariri aisee, mambo hubadilika.
Kilichobadilika ni mfumo tu wa kutoka sensa ya analojia na kuwa sensa ya kidigitali lkn taaratibu zote za ufanyikaji wa Sensa ni zilezile. Tuache kuzungumza/kuongea tusiyoyajuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…