Fafanua vzr mkuu,
Kwamba Kata ndiyo watatoa majina kwa nbs badala ya nbs ndiyo wawape majina Kata kwa hoja kuwa ni ili nbs wajiridhishe kuwa muombaji ni mkazi wa eneo husika.
Mkanganyiko wangu ulipo ni kwa nin nbs wawe na mashaka na muombaji kuwa mkaazi wa eneo husika haliyakuwa wakati wa kutuma maombi kuna fomu ilikuwa inajazwa na muombaji,wadhamini wake lakini pia uongozi wa serikali ya mtaa/kijiji kwa maana ya mtendaji wa mtaa.
Swali langu.
Mtendaji wa mtaa/kijiji aliwezaje kumsainia fomu muombaji na ikatumwa nbs bila yeye kujiridhisha kama muombaji ni mkaaji halali wa eneo husika na kama hiyo haitoshi akachukua nakala ya fomu hiyo na kubaki nayo ofisini kwake na sasa hao nbs bado warudi tena kutaka ushahidi wa ukaazi wa muombaji kwenye eneo husika?