Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Vipi ikiwa waombaji wote kwenye kata husika wanamakosa hayo au asilimia kubwa wapo hivyo watatumia na nafasi zipo wazi vigezo gani vitatumika ?
Umemuuliza swali zuri sana, atuletee majibu hapa kuna watu wanajifanya wajuaji sana aisee, muda ndio utakao amua ipi mbivu na ipi mbichi?
 
Kamisaa wa sensa
IMG_20220707_154314_510.jpg
 
Vigezo walivyotumia kukata majina ya waombaji ni
1. Sahihi ya mwombaji kutowekwa
2. Waombaji kuweka living certificate
3. Sahihi za wadhamini kutowekwa
4. Kutokata sehemu waliyoandika afikiriwe ama asifikiriwe.
5. Kutoweka mhuri wa mtendaji yeyote kata au kijiji.

NB. nenda uangalie copy za form yako ukiona umenusurika na hivyo vigezo ujue jina litatoka.
Kuna watu utumbo umeakata taa
 
Labda tume overthinking, maelezo yalisema makarani watafanyiwa usaili na watendaji wa mtaa,sasa wewe hapa ni kipi kigumu?
Majina yanatoka hapa soon then kama jina lako lipo utaliona kwenye ofis ya kata au ya mtaa
Baada ya hapo kinachofata ni usaili ambao watahusika watu wa kata husika. Baada ya hapo watendaji watawasilisha wajina nbs,mbona kwenye uchaguzi mkuu shughuli wanafanya watendaji tuwaamini tu.
NBS wako nyuma ya muda lolote linaweza kutokea, tuache muda uamue.
 
Vigezo walivyotumia kukata majina ya waombaji ni
1. Sahihi ya mwombaji kutowekwa
2. Waombaji kuweka living certificate
3. Sahihi za wadhamini kutowekwa
4. Kutokata sehemu waliyoandika afikiriwe ama asifikiriwe.
5. Kutoweka mhuri wa mtendaji yeyote kata au kijiji.

NB. nenda uangalie copy za form yako ukiona umenusurika na hivyo vigezo ujue jina litatoka.
Bakini nazo, si lazima.
 
Hiyo Ni nadharia Mkuu Wala usiwe na presha.
NBS hawawezi na hawana muda wa kuhakiki kuwa huyu MTU ni mkazi wa Kata husika Kwa Namna yoyote ile hasa ukizingatia muda umeenda Sana.
Na ndo maaana ili Zoezi la uhakiki linafanywa Kwa kiasi kikubwa na Watendaji wao ndo kila Kitu.
NBS wao uhakiki wao ni kuangalia zile taarifa ulizotuma ni Sahihi na zinaohana na TAARIFA za Watendaji.
NBS hawana ishu KUBWA hapo
Mchawi Ni Mtendaji Yeye Ndo Kila Kitu.
Daah, hapo sasa nimeelewa
 
Kamisaa wa Sensa Anna Makinda, amesema baadhi ya Watanzania wanapenda uongo kutokana na maneno ya uzushi yanayozagaa mitandaoni kwamba majina ya wasimamizi wa sensa hayatoki kwa sababu wameweka watoto wao, na kusema majina yakitoka waombaji wote wenye sifa watachukuliwa.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 7, 2022, mkoani Katavi, wakati akizungumzia suala hilo la kutangazwa kwa majina ya wasimamizi wa sensa.

"Tanzania tunapenda sana uongo, eti wameweka watoto wao nani kawaambia tumeweka watoto wetu, bado majina hayajatoka sababu tunafanya kazi kwa umakini," amesema Kamisaa Makinda

Aidha Mama Makinda, amewatoa hofu waombaji kuwa wote wenye sifa watachukuliwa kutokana na uhitaji uliotangazwa na serikali,

"Watu laki mbili na elfu tano ndio wanaotakiwa kwa ajili ya kazi ya Sensa ila mpaka sasa tumepokea maombi zaidi ya laki sita,".
JamiiForums-382760650.jpg
 
Back
Top Bottom