Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Na. Makao makuu ya Polisi – Dodoma,

Jeshi la Polisi nchini limewatadhadharisha wananchi juu ya uwezekano wa kuibuka kwa matapeli baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kutoa tangazo la ajira Disemba 1, 2022 kwa vijana wenye sifa za kuajiliwa na Jeshi hilo.

Hayo yalisemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Msime alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari kufuatia kutangazwa kwa nafasi za ajira za Polisi.

Alisema kuwa vijana, wazazi ama walezi wasikubali kurubuniwa na mtu yeyote, awe anajiita mtumishi wa serikali wa aina yeyote au mwenye cheo chochote au mtu mwingine yeyote yule atakayewaambia kuwa anao uwezo wa kukusaidia au anafahamiana na kiongozi fulani ambaye anaweza kukusaidia kupata ajira hizo nje ya utaratibu uliotangazwa au utaratibu mwingine utakaotolewa baada ya Disemba 27, 2022 ambayo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kuomba nafasi ya ajira.

Misime aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linasisitiza kama kijana unazo sifa zilizoainishwa katika tangazo la ajira ni vema ukafuata maelekezo yaliyoambatana na tangazo hilo na si vinginevyo.

β€œUkikiuka na kufuata maneno ya ulaghai wa matapeli watakao kuambia toa kitu fulani ili usaidiwe, itakuwa ni hasara kwako na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yako kwa mujibu wa sheria pamoja na tapeli mhusika,pale itakapo bainika” alisema Misime.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pale watakapo baini kuibuka kwa watu (matapeli) wa aina hiyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
 
Sahihi kabisa [emoji23][emoji23][emoji23] Zimamoto huwa sio ndefu sana. Uhamiaji Nadhani ni miezi 6 hivi
Kule unaishi kama mzuka mda wote mimi kuruta " mimi kuruta"

Mda wowote unaogopa kujichanganya ukaaga mashindano na asikwambie mtu hivi unajua maisha ya uoga ya kuwindana kama digidigi yalivyo ? [emoji3]


Ukiumwa kidogo malaria we tayari unfit , buti hujapiga kiwi we tayari ushaharibu [emoji3]


Ndio maana wakimaliza wakichomoka ccp wanakuwa wamevurugwa morali kama zote usiombe ukutane na kisanga cha askari mpya huo utukutu wako utaisha
 
Kwaiyo km ukupitia mafunzo ya jkt kwa mujibu wa sheria imeisha iyo
Kila siku tunasema humu ndani mujibu wa sheria ile ni jkt umepewa cheti cha jkt

Sasa wewe usiombe useme mimi ni mujibu wa sheria shauri yako

mbona mifano ipo mingi ya mujibu wa sheria kupata nafasi kunguru wa Manzese alikuwa mujibu wa sheria kwenye ule uzi wa ajira za utumishi alisema amepoteza nauli sana Dodoma sema sijui mwamba alisomeaga nini huku kwenye majeshi hatimaye kabahatisha


Halafu ukichinguza wengi ambao wanaombea cheti cha degree hizi ajira za majeshi ni mujibu wa sheria na kwenye list ya kupata wapo
 
Nimecheka saaana kudadeki [emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…