Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

ninoma mkuu wangu,sema watu wanaibuka na hoja za vijiweni
Watu wanaongea humu utasema wamepiga depo la CCP na kiwira.

Niwaulize tu lini mliwahi kuona askari magereza yupo operation yoyote mfano ile ya Kibiti au Mtwara?[emoji1]
Ndio mjue sasa PT ni baba lao hata huko CCP mziki wao si wa kitoto. Operation zote za ndani ya nchi hadi nje wanaenda Jw na PT.
 
Mahovyo hovyo yapo mzee mwishoni ndio wanalegeza ile miezi ya mwanzoni ni mwendo wa mabio point A-B huku unaimba "Mimi kuruta" kuamka sasa ni saa 6 kasoro za usiku miezi yote 9 mnaenda mabio na siku za wikendi mnakimbia mabio marefu(induarance) kuna miezi kadhaa ya kutembea kikamavu yani hatua kumi za kutembea unatakiwa uzitembee kwa sekunde 3 noma hiyo mjomba wenyewe wanaiita 'three-twenty' kama sijakosea. Na ukileta mapuuza ya kuacha kufanya hayo maovyo hovyo unaweza pepea.


Nimeambiwa na pot aliyetoka juzi kati huko CCP.
 
Humu ndani Wapo pia waliopiga CCP ..ndio maana tunaziita zote hizo zote hizo ni lonja
 
Mimi haya binafsi sihesabii kama maovyoovyo...mabio..kuimba mimi kuruta naona ni kama wajibu tu wa kawaida ambao unatakiwa kuutimiza. Kwangu mimi maovyoovyo nayachukulia yale mambo ya madoso yasiyo na msingi...yani sjui kwenda kula ..afande anawepeleka kwa mwendo mbaya...mara kichura...mara kuroll kama yale ya jkt...haya ccp naambiwa hakuna hizi bugudha especially wakati wa kula.
 
Kwani vazi la uhamiaji ni wapi limeruhusiwa kuzurura nalo ?
 
Mimi sijawahi kupenda mahovyohovyo yasiyo na msingi kama hayo ya kupelekana kula kwa mwendo mbaya ndio maana kwangu mm naona course ya polisi ni kozi ya kawaida endapo tu utatimiza wajibu wako na kufuata sheria.Hayo mambo ya kuimba mimi kuruta ni unajitoa akili tu tena unaimba kwa Sauti na morali hamna atakayekugusa...mabio unatimia unaenda..vipindi class unaenda. Wenzangu na mimi wa tengo ukilipata unalipalilia vizur hadi Waone umuhimu wako....unaenjoy maisha huku unasubiri miezi yako miwili ya msoto porini kusipokuw na tengo
 
Iliyopita ilikuwa mwaka jana mwishoni kwenye mwezi wa 11
Mwaka huu tangazo lilitoka January 1 deadline ikawa January 14. Majina ya interview wakatoa January 28. Majina ya waliopta kazi wakatoa February 22 .

Leo ndio siku ya mwisho UT. Uwezekano wa kutoa majina ya kuitwa usaili ni kati ya tarehe 12/13 kama mambo hayatabadilika.
 
Porini ni miez miwili tu..?
Kila siku kuamka saa 6 kulala ni saa ngap sasa
 
Chakula cha jioni ni saa 12 jioni. Ukimaliza kula hapo ni utawala wako binafsi utajua mwenyewe kama utalala au utakuw unafanya nn. Ila saa 6 usiku kuamka siku inaanza. Porini kulala ni saa 4 usiku kuamka saa 11 asubuhi.
Huu muda wa kulala upo vizuri sana.

Kiukweli kwenye kozi mchawi usingizi aisee..

Yaani ni bora unipige doso la kutosha ila unipe muda mwingi wa kulala.

Mkuu Dystonia7, Vitengo huanza kugaiwa mwezi wa ngapi tangu mripoti kambini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitengo rasmi ni huwa baada ya wote kumaliza pori. Ule mwezi mmoja wa maandilizi ya kupass out ndio kuna kuwa na vitengo official. Kabla ya hapo watu huwa wanajiongeza wenyewe tu kupunguza makali ya course. Kwa mfano pale kuna Hospital inahudumia Raia wengi tu so madaktari na wataalamu wa huwa wanasaidia kutoa tiba inakuw kama tengo Lao 😂. Pia watu wa mifugo wanasaidia huko ilipo...mafundi/ maengineers n.k
 
Mkuu na sisi watu wa Finance hamna vitengo [emoji28][emoji28]?..

Maana sio poa.[emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…