Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Ukweli mchungu ambao hatuupendi na hatutaki kuambiwa.
 
Nchi yetu kwenye vyombo vya ulinzi Polisi alipaswa kupewa maokoto makubwa kuliko ata mwanajeshi
 
Kwanini ndugu.?

Hivi unajua kazi ya jeshi ni kuweka roho rehani.

Kazi ya kulinda mipaka ya nchi na kulinda amani sio shughuli ndogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jeshi kweli linapiga kazi lakini kaka Pt kwa bongo wanahenyeka sana

Vitisho vya usalama sio vingi sana kwa nchi yetu, Naandika nikiwa nipo mpakani mwa Tz
 
Jeshi kweli linapiga kazi lakini kaka Pt kwa bongo wanahenyeka sana

Vitisho vya usalama sio vingi sana kwa nchi yetu, Naandika nikiwa nipo mpakani mwa Tz
Mkuu.

Vitisho vya usalama sio vikubwa nchini kwasababu jeshi letu limetengeneza 'fear factors' Kwa waasi na maadui na hii ni kutokana na kazi kubwa wanayoendelea kuifanya.

Jeshi letu limejizolea sifa kubwa na ndio maana hata UN wanatupa mission nyingi za peace keeping.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mchungu ambao hatuupendi na hatutaki kuambiwa.
Ila kiuhalisia jamaa amesema ukweli maana mshahara wa million 1 utaishi maisha ya middle class tu
Kuna kazi au biashara ukifanya unapata zaidi ya hizo ..yani kuna mashirika staff mmoja allowance anayopewa ni sawa na mshahara wa mtu serikalini
Acha tu hvyo dereva wa abiria kukunja million kwa mwezi ni kugusa tu...
all in all BIASHARA NDIO INA HELA SANA
Tunapokua tumeajiriwa tujiongeze zaidi na ishu zingine
 
Yeah huu ni ukweli na system za ajira zimewekwa kutudumaza akili
 
Kumbe Maokoto yanaeleweka kiasi chake.

Vipi kuhusu kada kama za Engineers? I.e Civil Engineers au police hawachukuagi wahandisi
Polisi maokoto yapo ukiachana na mshahara na hizo nyingine kuna posho ya vitengo.mfano ukIbaki kuwa mkufunzi kwenye shule zao unapata posho ya 50% ya mshahara na vitengo vingine kama forensic ,kuna asilimia za posho zao nao. nna rafiki angu ana diploma tuu ila naona mambo yake ni mazuri kamaliza depo iliopita sahizi ana kiwanja kigamboni huko na pikipiki mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Yeah inaonekana sio pabaya maokoto kwa maisha yetu ya kitz inatosha kuendesha maisha ya kila siku na focus kwenye maendeleo madogo madogo mtu hawezi kukosa.
 
[emoji23][emoji23] kiwanja na pikipiki mbili kwa sifa unazompa sio sawa..!!

Nina wajua madereva bodaboda wenye nyumba mbili na bodaboda zaidi ya 6 na wanasoma mpaka form 3 au hajaenda shule Kabisa
 
[emoji23][emoji23] kiwanja na pikipiki mbili kwa sifa unazompa sio sawa..!!

Nina wajua madereva bodaboda wenye nyumba mbili na bodaboda zaidi ya 6 na wanasoma mpaka form 3 au hajaenda shule Kabisa
Mafanikio ni hatua kiongozi

Umeambiwa kamaliza depo iliyopita ivyo hana muda mrefu kazini na hata ujui ana wategemezi wangapi nyuma yake ambao wote wanautazama mshahara wake.

Hii ndio tabu wanayokutana nayo hata graduate kuanza kuwalinganisha na watu walioanza kutafuta maisha kwa zaidi ya miaka saba mtaani mnataka kumlinganisha na graduate alietoka chuo mwaka mmoja uliyopita

Mwisho wa siku mnawapa presha sana vijana kwenye utafutaji waacheni kila mtu apite na njia yake.

Lengo liwe ni moja kupambana na adui UMASIKINI na sio kupambana sisi kwa sisi nani yupo juu na nani yupo chini.

Vijana wa miaka 20-30 msichanganywe na hii presha ya mitandao.
 
Nini maana ya uzalendo?

Hiyo 500k ni ndogo sana ila ukiwa na akili unatoboa halafu watu watabaki wakisema "Polisi wala rushwa,wanamiliki mali kubwa kuliko mishahara yao".

Polisi mishahara yao ni midogo mno hata serikali inajua(sijui kwanini hawawaboreshei) ila isiwe sababu yakufanya watu wasifanye kazi ya polisi/kutumikia nchi kupitia Jeshi la Polisi.Polisi ni wazalendo na ndio maana hawajawahi kugomea maelekezo ya serikali eti kisa wanalipwa 'kiduchu' ukilinganisha na kazi yao ngumu.

Kuhusu ulaji rushwa hiyo inategemea tamaa zako na kuwa na moyo ambao haujali makatazo ya Mungu,sio polisi wote wanakula rushwa bali ni baadhi tu.Pia nataka niwaambie 'hakuna mkate mgumu mbele ya chai' na ndio maana hata wakuu wa taasisi,watumishi wengine katika taasisi nyinginezo pia wanakula rushwa.

Hivyo niwape rai wadogo zangu ombeni kazi ya Upolisi pale fursa inapotokea mkiendako mukafanye kazi kwa weledi,matendo maovu ni ya mtu mmoja mmoja na wala si ya taasisi nzima,polisi ni kazi kama kazi nyingine:mkiajiliwa ndani ya polisi mtapata exposure;mtaenda nje ya nchi kuhudumu katika nchi mbali mbali kama walinzi wa amani(individual police&Formed police unit/FPU) huko mtapata hela yakutosha ya kufanyia maendeleo mrudipo nchini.Pia wengine(wataalam) mtahudumu katika polisi ya kimataifa(Interpol) napo mtapiga pesa halali ya maana.

Polisi ni kazi nzuri tofauti na tunavyoibeza,nina ushuhuda juu y hili.
 
Mfumo wa Ajira Bongo ni magumashi matupu sana nilikuwa najiuliza why watu wako Furatsrated sana hasa wakiingia katika Payroll ya GVT mwezi wa 4 tu huu ndani ya GVT nimepata majibu! Tena uwe na HESLB utasanda tu
Acha tu kuna mwana yupo Dar ni polis na yy ni mzanzibar ananiambia kila cku yupo job Hana hata muda wa mapumzik weekend Kam atajiongeza kiupande mwengin yeye ni kutegemea salary tu afadhal anapata Hela ya lindo maan yeye kila cku yupo bank anasem Kam anapat muda bas angejishuhulish na mambo mengine maan ana ujuz wake lkn kinachomgharim hapat chance han mapumzik
 
Mwambie afanye 'namna' kwa wakubwa.

Kuna mwanangu alikua wilayani,alikua busy na malindo ya bank, Mahakamani na escort,japokua wanalipwa ila mwishowe akachoka maana hata muda wa kugegeda ikawa ishu.

Huku na huku 'akapiganisha' akapata order ya kwenda Kikosi cha mbwa na farasi.

Anasema kitengo cha mbwa na farasi ni bata kwenda mbele,,Kila siku ni weekend.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa konstebo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…