Nini maana ya uzalendo?
Hiyo 500k ni ndogo sana ila ukiwa na akili unatoboa halafu watu watabaki wakisema "Polisi wala rushwa,wanamiliki mali kubwa kuliko mishahara yao".
Polisi mishahara yao ni midogo mno hata serikali inajua(sijui kwanini hawawaboreshei) ila isiwe sababu yakufanya watu wasifanye kazi ya polisi/kutumikia nchi kupitia Jeshi la Polisi.Polisi ni wazalendo na ndio maana hawajawahi kugomea maelekezo ya serikali eti kisa wanalipwa 'kiduchu' ukilinganisha na kazi yao ngumu.
Kuhusu ulaji rushwa hiyo inategemea tamaa zako na kuwa na moyo ambao haujali makatazo ya Mungu,sio polisi wote wanakula rushwa bali ni baadhi tu.Pia nataka niwaambie 'hakuna mkate mgumu mbele ya chai' na ndio maana hata wakuu wa taasisi,watumishi wengine katika taasisi nyinginezo pia wanakula rushwa.
Hivyo niwape rai wadogo zangu ombeni kazi ya Upolisi pale fursa inapotokea mkiendako mukafanye kazi kwa weledi,matendo maovu ni ya mtu mmoja mmoja na wala si ya taasisi nzima,polisi ni kazi kama kazi nyingine:mkiajiliwa ndani ya polisi mtapata exposure;mtaenda nje ya nchi kuhudumu katika nchi mbali mbali kama walinzi wa amani(individual police&Formed police unit/FPU) huko mtapata hela yakutosha ya kufanyia maendeleo mrudipo nchini.Pia wengine(wataalam) mtahudumu katika polisi ya kimataifa(Interpol) napo mtapiga pesa halali ya maana.
Polisi ni kazi nzuri tofauti na tunavyoibeza,nina ushuhuda juu y hili.