Oktoba tarehe za mwanzo mwanzo mbivu na mbichi mtazijua..
Japo nasikitika kuwaambia vigezo vitawaangusha wengi sana watu wametuma maombi MM hata wasio na sifa,yaani mtu hana sifa hata moja labda sifa ya kuwa na Shahada au Stashahada,Astashahada tu.
Wapo walioandika barua zao kwa kuchapa kwa kompyuta,wapo walioambatisha vyeti vinatofautiana majina mfano mtu leaving ya kidato cha 4 anaitwa Anna Masesa ila cheti cha Shahada anaitwa Anna Richard Masesa,wengine barua za utambulisho hajaweka sasa hapo lazima upigwe chini tu.
Ila wapo walio smart sana mtu kaweka kila dokumenti aliyotakiwa kuiambatisha,barua safi kaandika,kaweka passport 3,kaweka kivuli cha namba au kadi ya NIDA,kaweka barua ya utambulisho,mwingine kaweka hadi barua ya tabia njema kutoka PT,vyeti vyake vya elimu viko na majina sawa na vimethibitishwa na mwanasheria,fomu ya hospitali kaweka yaani safi kabisa.