Kabla ya ajira za upolisi mwaka 2021 nilikuwa na ndugu mkubwa tuu huko juu polisi.... Alinisisitiza kuwa ajira zikitoka nimstue na atalishughulikia!!! Baada ya ajira kutoka nikamstua akichonijibu ni kuwa nitapata tuu bila hata yeye, hakuuliza majina wala kikosi wala ninii akapita hivi.!!!
Mwanzoni mwa mwaka 2022 nikamfahamisha mtu mmoja ambaye sio ndugu wala nini shida yangu ya kutaka kujiunga huko, nae ni polisi na ni mmama... Alisikita sana nimechelewa kumwambia kwani alipewa nafasi tatu na hakuwa na mtu mwenye vigezo ilimbidi azikatae..!!
Lakini aliniambia nisife moyo zikitoka nyingine nimtafute!! Haya sasa zinetoka yeye ndio alianza kwanza kunitafuta, kuniuliza details zote na kuahidi kunishughulikia!! Hadi sasa naona mwanga!!
Huyu mtu ni mtu baki na ameniona mara moja tuu physically..na hapo ni upande wa PT.
The same thing kwa vyombo vingine...
Ndugu bwa kweli sio damu wakuu.. hawa ndugu wa damu ukitoa wazazi mara nyingibwao tuu ndio wanapenda kuwa juu!!