SoC04 Nafasi za Mawaziri zinazohitaji ridhaa ya Wananchi

SoC04 Nafasi za Mawaziri zinazohitaji ridhaa ya Wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Mar 21, 2024
Posts
5
Reaction score
3
Habari wadau,

Kulingana na taratibu, sheria na kanuni mbalimbali za nchi hii nafasi za mawaziri huteuliwa na mheshimiwa raisi.

Lakini siku ya leo napenda kutoa maoni yangu juu ya nafasi tano za mawaziri ambazo zinahitaji umakini wakati wa uteuzi na ikiwezekana uanzishwe utaratibu wa kupata ridhaa ya wananchi. Kwa maoni yangu nafasi hizi ni muhimu sana kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Zifuatazo ni nafasi hizo;
1. Waziri wa katiba na sheria.

Hii ni nafasi nyeti inayoshikilia maendeleo ya taifa. Taifa lenye maendeleo mazuri linahitaji kuwa na sheria bora na katiba bora inayoweza kulinda na kupigania maslahi ya wananchi wake. Kama taifa tunahitaji kiongozi atakayeshika nafasi hii awe na uwezo wa kusimamia utunzi wa sheria bora na zenye kulinda maslahi ya wananchi.

Sifa za mtu anayefaa kuwa waziri wa katiba na sheria
1. Awe na ufaulu mzuri katika masomo ya sheria.
2. Awe na uwelewa mpana juu ya katiba na sheria
3. Afahamu vyema sheria za kimataifa na haki za binadamu.

2. Waziri wa Jinsia wanawake na watoto
Hii ni wizara ya muhimu sana katika maendeleo ya taifa letu. Kutokana na changamoto za hivi karibuni kama vile ushoga, usagaji, unyanyasaji wa kijinsia na kingono, ni maoni yangu kwamba kuwepo na utaratibu wa kuchagua mawaziri katika sekta hii.

Sifa za mtu anayefaa kuwa waziri wa jinsia, wanawake na watoto.
1. Awe na taaluma juu ya jinsia na usawa.
2. Anatakiwa kufahamu changamoto zinazowakabili wanawake na watoto.
3. Awe na uwezo wa kutunga sera zinazo linda usawa wa kijinsia katika jamii.

3. Waziri wa Fedha
Ili kuweza kuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo inafaa sana kama taifa tuwe na kiongozi mwenye uzoefu katika sekta ya uchumi na fedha ili kufikia malengo.

Sifa za mtu anayefaa kuwa waziri wa fedha na uchumi
1. Awe na uwelewa juu ya mifumo ya uchumi wa dunia
2. Awe na uzoefu juu ya kutatua changamoto zinazohusiana na uchumi kama vile ukosefu wa ajira.
3. Awe na ujuzi maalumu wa kutatua migogoro wakati wa majanga. kwa mfano wakati wa milipuko ya magonjwa kama COVID 19.
4. Awe na uwezo wa kufuatilia kwa ukaribu namna kodi za wananchi zinavyotumika katika kufanya miradi ya maendeleo.
5. Awe na uwezo wa kutunga sera rafiki kwa vijana.

4. Waziri wa ulinzi na usalama.
Usalama wa nchi hutokana na siasa zinazopigwa lakini pia hutokana na aina ya kiongozi anayeshika ofisi hio. Ili taifa liwe na maendeleo ulinzi ni muhimu sana katika maisha ya watu, hivyo basi ni maoni yangu kwamba waziri wa sekta hii achaguliwe na wananchi.

Sifa za mtu anaye faa kuwa waziri wa ulinzi.
1. Awe amepata mafunzo na elimu kutoka jeshini
2. Awe na taaluma inayohusiana na diplomasia
3. Anafaa kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za vyombo vya ulinzi na usalama. kwa mfano changamoto za polisi (mishahara na vitendea kazi).

5.Waziri wa mambo ya nje.
Hii ni sekta muhimu sana katika taifa letu la tanzania , Mahusiano mazuri na mataifa mengine huchagwizwa na aina ya kiongozi atakaye pata nafasi ya kuongoza sekta hii. Ni maoni yangu kwamba waziri wa sekata hii pia achaguliwe na wananchi.

Sifa za mtu anayefaa kuwa waziri wa mambo ya nje.
1. Awe na taaluma juu ya diplomasia
2. Awe na uzoefu juu ya sheria za kimataifa
3. Awe na uwezo wa kutunga sera bora za kujenga mahusiano mazuri na mataifa mengine.

Hitimisho: Kama wananchi ni muda muafaka wa kutaka kushiriki katika kuteua nafasi mbalimbali za mawaziri ambazo huonekana ni nyeti. Hii itasaidia sana kuwajibisha viongozi hawa pindi wanapofeli kutekeleza majukumu yao. Faida nyingine kubwa ni kwamba tutapata watu sahihi wakusimamia kila sekta.​
 
Upvote 2
Kama wananchi ni muda muafaka wa kutaka kushiriki katika kuteua nafasi mbalimbali za mawaziri ambazo huonekana ni nyeti. Hii itasaidia sana kuwajibisha viongozi hawa pindi wanapofeli kutekeleza majukumu yao. Faida nyingine kubwa ni kwamba tutapata watu sahihi wakusimamia kila sekta.
Wazo zuri, iwe kateuliwa iwe kachaguliwa muhimu atosheee kwenye nafasi yake. MERITOCRACY
 
Back
Top Bottom