Nafikiri hii ndiyo sababu ya matajiri kuitwa katili wasiyo na utu

Kumiliki pesa kunahitaji akili kubwa sana.

Kumiliki pesa kunahitaji uwe na roho ngumu!
Kumiliki pesa siyo suala la mchezo mchezo!
 
Duh ebhanaee uchumi wa kati juu kabisa huu kwa watz wengi dogo ana uchezea 😄
Aisee gharama zote ingekuwa mm nisingesubiri hata mfungo uishe
Ujue huyu alikua ni mwanzoni kuingia, nilipoona hali hii nikam team in mtu mwingine. Sio kama ajira, but kujitolea ao nikamwambia utalipwa 160k kana nauli tu za kwenda na kurud kazin lakin ofisn vitu kama chai na lunch na maji ya kunywa ofisni vipo, imagine huyu ni university graduate ila ana juhud kushinda huyu kijana ambaye ana diploma tu. Ndio maana nafikiri acha nimuondoe tu, kisha nimpromote huyu mwingine
 
Nipo hapa salesman mwenye weledi, naomba hiyo kazi
 
Hapo mna deal na ishu gani?
 
Mkuu hawa madogo wa 2000 kazi wanayoweza ni kuangalia Simba na Yanga na Kubet Tu.

Hawana akili.

Sisi ktk Lika lao tulikuwa tunasaidia hadi mahitaji ya familia na kule wadogo zetu.

Tulikuwa tunalima vibarau kwa ujira mdogo( kusogeza maisha, kubeba mbao, kupasua kuni, kuuza miwa.

Hawa wa leo ni mtihani sana.

Nimeweka ka ofisi ili namimi niitwe bosi kakuuza huduma tu.

Nikamwaga pale milioni 4.

Ofisi ina uwezo wa kuingiza elfu 20 kila siku ila dogo akawa ananiletea elfu 3.

Nikamtimua mara anaenda kucheza mpira muda wa kazi

Kazi yenyewe anaanza saa tisa alasiri hadi saa tatu usiku.

Nikamweka Mdogo wangu wa kuzaliwa amekaa mwezi mmoja tu sasa hivi ananiletea elfu 15 daily.
 
KWakwel ni mtihani sana brother. Mtihani sana
 
Look for another smart young man out there, wapo wengi ambao ni very talented and dedicated, achana na huyo asiyejitambua!
 
Mimi naona makosa mengi yako upande wako. Huyo dogo yuko sahihi kabisa kwasababu kachagua kuwa mpumbavu ila wewe unamlazimisha aache kufanya kitu anachokipenda. Kwanini unamlazimisha Nyani aamini kuwa asali ni tamu kuliko ndizi? Kimsingi makosa yako ni haya;
1. Unaleta usomi uchwara kwenye biashara. Kiswanglish chako ni ishara ya kwanza. Ingia kwenye biashara bila kuleta mbwembwe za usomi hata kama ni msomi. Acha kazi zikutambulishe.
2. Hiyo sababu namba 1 inafanya utumie gharama kubwa kuendesha biashara yako. Watu wanne wa kazi gani wakati mnaweza kuwa wawili tu mkapiga kazi? Ukitaka wengine si unawapa tu kazi za deiwaka?
3. Bado biashara yako sio kubwa. Bado unajitafuta. Hii ndo sababu umekuja kulia hapa kwasababu ya hivyo vichomi vya gharama zinazokuandama.
4. Technically umekosea sana kumlipa sales man mshahara. Hapo anachostahili ni hiyo 7000 ya nauli na commission. Halafu commission ya 40% kivipi? Ina maana huyo dogo ni shareholder? Hii kama sio chai basi wewe ni mjinga mno na inabidi utafute mtu akufundishe.
5. Unafanya show off za kujifanya ni mtu mwema. Huwa tunasema usijifanye mkristo kuliko Yesu mwenyewe.
6. Ni mwoga wa kufanya maamuzi magumu. Ukiendeleza huo uoga utafilisika. Umekubali hadi dogo akudharau.

NB: Nampongeza huyo dogo kutafuna hela zako hadi akili ikukae sawa.
 
Sina shaka yoyote Uzi huu umeandikwa na Boss msomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…