Nafikiri hii ndiyo sababu ya matajiri kuitwa katili wasiyo na utu

Nafikiri hii ndiyo sababu ya matajiri kuitwa katili wasiyo na utu

Ofcz i dont pay him much. Japo kibiashara ni pesa nying, maana uki compare his value na what am paying him bado ni pesa nyingi sana

  • 300,000/= monthly salary
  • 7,000= daily marketing transport
  • 40% commission on spot kwa kila sale anayofanya
  • 3-5% salary incrementt kwa kila sale anayoifanya
  • lunch
Kwa malipo haya mkuu,nadhani wale wanaotembeza mabeseni wakiona watajisikia vibaya sana.

Fikiria mtu anazurula 50kms na ili alipwe kwa mwezi ni mpaka mzigi wote uwe unakwisha.😀😀😀

Sorry labda dogo kuna namna nyingine anakufaa hujatuandikia hapa.
 
BRaza ahsante kwa ushauri japo umetumia lugha kali sana isivyo lazima.
kwanza kabisa nikiri mpaka kulileta hapa ni dhahiri linaniumiza sana kichwa ndio maana hapa nikaona ni mahala sahihi kabisa.

sio kwamba nafanya mbwembwe, hapana. Najaribu tu kufuata taratibu za kazi na pia ku apply proffesionalism kwakua hii ni biashara ya tofauti kidogo mkuu wangu, una deal na institutions so watu wako wanafanya kaz kuna namna wanapaswa kuwa na kuna namna wanapaswa kuwa treated.

Hii uko sahihi, na moja wapo ya njia niliamua ku come up baada ya kuumiza kichwa ni kuwa na sort of dayworker lakin kwangu imekaa tofauti. I started with an oversea person ambaye yeye ana kaz zake lakin anafanya pia kaz na mimi kwa namna tulivyo arrange na njia hii nimeanza kuona matokeo yake

SIkupingi kabisaa mkuu. Ndio maana nikaleta hoja mezani

SIo chai.
40% ni one time sale commision, analipwa mara 1 tu. Mfano amefanya sale kwa mteja ambaye tunaingia mkataba wa kufanya nae kasz kwa gharama ya 100,000/= kwa mwezi, kama ofisi namlipa 40,000/= kama commision. Yeye sio share holder japo katika hii sale ya 100k aliyo fanya nitapa icrememt ya 5% kama nyongeza ya mshahara wake kwa miaka mi 3 as long as mteja huyo haitatokea kuvunja mkataba

sifanyi show off chief. Kama umekwazika nisamehe sana maana sio lengo. Kumbuka pia tumetofautian, ulivyo sivyo mwingine anaweza kuwa. Tusaidiane kupeana mawazo badala ya kutoleana lugha zisizofaa

inaweza kuwa kwel. Moja ya kitu ambacho nakiri nakosa ufanisi ni katika suala zima la managent. Nature yangu ni kwamba napendelea kufanya kaz na watu wenye akilo wanaojua nini wanatafuta ili kupunguza kufuatiliana sana. Huo muda nikiri huwa naona kama bora ni invest katika kufanya mambo ya msingi zaidi kuliko kukufuatilia wewe. Nafikiri kaz yangu ya kwanza ilini athiri, sipendi kufuatiliwa katika kaz na matokeo yake ndio haya sasa huwa na assume mtu hatakiwi kusimamiwa kwenye majukumu yake ambayo mwisho wa siku analipwa kuyafanya. Kwann nikulipe na bado nikufuate nyuma nyuma?

Sawa.
Lugha kali ndo utakayoelewa kirahisi. Mimi sio Mtakatifu Mathayo kwamba niongee kwa lugha ya kubembeleza. Punguza hizo mambo za professionalism. Nenda jinsi watu wanavyotaka. Inawezekana hata kazi nzuri unazikosa kwa kuendekeza huo utumwa wa professionalism huku ukipuuza codes muhimu za kitaa. Decision makers wa hizi taasisi za kibongo wana lugha zao za kipekee kaa chini ujifunze. Unavyosema una udhaifu kwenye management jua kabisa anguko lako haliko mbali endapo hutabadilika. Saa nyingine FUMANIZI HUIMARISHA PENZI. Punguza huo utakatifu uchwara. Huyo dogo kata maslahi yake yote mwachie nauli na lunch tu. Kama HAWEZI FUKUZA WEKA MWINGINE.
 
Lugha kali ndo utakayoelewa kirahisi. Mimi sio Mtakatifu Mathayo kwamba niongee kwa lugha ya kubembeleza. Punguza hizo mambo za professionalism. Nenda jinsi watu wanavyotaka. Inawezekana hata kazi nzuri unazikosa kwa kuendekeza huo utumwa wa professionalism huku ukipuuza codes muhimu za kitaa. Decision makers wa hizi taasisi za kibongo wana lugha zao za kipekee kaa chini ujifunze. Unavyosema una udhaifu kwenye management jua kabisa anguko lako haliko mbali endapo hutabadilika. Saa nyingine FUMANIZI HUIMARISHA PENZI. Punguza huo utakatifu uchwara. Huyo dogo kata maslahi yake yote mwachie nauli na lunch tu. Kama HAWEZI FUKUZA WEKA MWINGINE.
Hili nitalifanyia kazi kamanda
 
Madogo wengi hawajitambui...nilikuwa nao mimi wawili ofisini kwangu, nilianza na mmoja wakati namwajiri alikuwa peke yake alikuwa akifanya vzr sana nikaona kama ana overwork( kosa hili) nikamwambia amlete mwenzie wawe wawili daaah kilichonikuta sasa....kwanza wakawa na kiburi kwangu hadi watejaa....wakaanza nipiga kwenye mahesabu nikiwauliza wanasema hawajui pesa zinavyopotea...mwisho wakanipiga loss....hapo ndipo akili iliponikaa na kuwapiga chini...usicheke na nyani kwenye pale unapopatia ugali hawana maana binadamu.
 
Nilikuwa na akili kama za kwako mpaka nilipokutana na huu msemo “Siku Simba akimuonea huruma Swala, ndiyo siku atakufa njaa”

Kumfundisha kazi mtu ni muhimu sana maana hakuna aliyezaliwa anajua, lakin lazima umfundishe mtu anayeipenda kazi yake, mwenye nidhamu na anayeweza kuijua mipaka yake

Zingatia KUIPENDA KAZI
 
Nilikuwa na akili kama za kwako mpaka nilipokutana na huu msemo “Siku Simba akimuonea huruma Swala, ndiyo siku atakufa njaa”

Kumfundisha kazi mtu ni muhimu sana maana hakuna aliyezaliwa anajua, lakin lazima umfundishe mtu anayeipenda kazi yake, mwenye nidhamu na anayeweza kuijua mipaka yake

Zingatia KUIPENDA KAZI
Nimekusoma chief.
 
Ofcz i dont pay him much. Japo kibiashara ni pesa nying, maana uki compare his value na what am paying him bado ni pesa nyingi sana

  • 300,000/= monthly salary
  • 7,000= daily marketing transport
  • 40% commission on spot kwa kila sale anayofanya
  • 3-5% salary incrementt kwa kila sale anayoifanya
  • lunch
Una uhakika huyu dogo Huwa anaenda marketing atakuwa akishachukua buku 7 anarudi gheto kulala
 
Nimesoma post nzima nimebaki kushangaa.

Hivi hawa generation Z wanaweza hasa kitu gani ?

Maana naona maturity kwa generation yao inapungua sana..

Miaka ile in our early 20's tulikua wanaume kabisa na wenye uwezo wa kuchanganua mambo na kufanya maamuzi mazito na kwa usahihi .

Nilipambana from the scratch hadi kutimkia majuu na kuanza moja ugenini bila kuwa na mtu hata 1 ninayemjua .

Leo hii mostly kws malalimiko nayoona kwa hawa generation Z na toddlers ni ndogo sana kwamba wao wanaweza kuongea, kutembea, kusoma na kuandika ila kimaamuzi naona kama bado sana.

Hawa vijana wa 20's naona wanaweza ngono, pombe, Tiktok, bangi , nk.
 
Nimesoma post nzima nimebaki kushangaa.

Hivi hawa generation Z wanaweza hasa kitu gani ?

Maana naona maturity kwa generation yao inapungua sana..

Miaka ile in our early 20's tulikua wanaume kabisa na wenye uwezo wa kuchanganua mambo na kufanya maamuzi sahihi .

Tulipambana from the scratch hadi kutimkia majuu na kuanza moja ugenini bila kuwa na mtu hata 1 ninayemjua .

Hawa 20's wanaweza ngono, pombe, Tiktok, bangi , nk.
Inasikitisha sana kaka. Tunawasaidiaje sasa?
 
Habari wanajukwaa,

Heri ya Kwaresma kwa ndugu zangu wakristo.

Ramadham Kareem kwa ndugu zangu waislam.

Kama ilivyo kwa wengi, katika harakati za upambanaji unajikuta una team up na wadau kadhaa katika kujaribu kuona ni namna gani mnaweza mkayafikia malengo kwa ukubwa, haraka na unafuu. BAsi na mimi ni mmoja wapo.

Nafanya biashara ya kuuza huduma. Nilianza alone lakin baada ya muda nikaona ni wakati muafaka kuongeza nguvu kazi tusaidiane majukumu. Nikapata kijana ambaye yeye kazi yake kama alivyoji profile ni Sales person. Nikamchukua nikamuweka ofisini tuanze maisha ya kushirikiana majukumu.

Alikua anafanya kaz kwenye moja ya miradi maarufu tu inayoendelea hapa jijini Dar es salaam, project ya wachina. Baada ya ku discuss terms na conditions tukaanza kazi. Tulikubaliana kuwa ni jukumu langu;
  • Kumuwezesha vitendea kazi
  • Nauli kila siku akiwa sokoni
  • Mshahara kwa mwezi
  • Commission (kubwa sana)
  • Bonus /nyogeza ya mshahara kulingana na anavyo perform majukum na kwakua sales is about numbers so iko waz anaweza kabisa aka predict baada ya muda gani atakua na nyongeza kiasi gani
  • Mawasiliano
Hayo ni haki yake kabisa. Sambamba na hayo tukawekana waz kabisa kuhusu wajibu wake pia ikiwemo
  • Target (ndogo sana ya kupata maximum 2 sales per month - 30 days)
  • Ku submit report (daily and weekly), nk.
Niwe mkwel kijana hakuanza vibaya lakini pia hakua vizuri kama ambavyo nilifikiri au kama vile alivyojipambanua. Nikaona sio tatizo sana, nitam coach. Na tukawa tuna kwenda vizuri kawaida.

Sasa kiasili, mimi sio wale watu ambao ni "Bossy type" japo nina u serious wangu wa kutosha tu. Napenda sana as long as work is involvesld, kuwa karibu na team players wangu. Kwakifupi huwa si entertain gap between me and my guys (ninao wa 4, office admin, tech assistant, sales guy na mmoja ambaye ni oversea sio office based).

Sasa baada ya muda kupita naona kijana amekua haeleweki na performance yake honestly hainiridhishi kabisaaa and inside my heart am deeply dissapointed amd am really thinkimg of what to do.

Kijana wa sales
  • Ja meet target. Yan ni 0%
  • mchelewaji ofisini
  • Hapokei simu hata iweje na anajua simu zangu ni strictly ni za kazi, ukitaka kuwasilana nae ni text tu kama yuko nje ya ofisi
  • Hatoi taarifa kama atachelewa, kwakifupi anaweza ondoka leo jion kaniacha ofisin (maana ninkawaida yangu kufanya kaz mpaka late hours) na akaja kesho akanikuta (ni kawaida yangu saa 12 asubh niko ofisni) , na hapo yeye kaja kachelewa but hakuna maelezo anakupa, ofcz huwa siulizi.
  • Hatumi report za kazi, kuna time nakua na kaz nje ya ofisi au nje ya Dar hata kwa week 1, hivyo hatuonani lakin hutaona report mpaka upige kelele kwamba nataka report.
  • Na unapokua mkali (kitu ambacho sikipend japo nakiweza) , basi dogo sio muoga kabisaa anabishana na wewe kana kwamba wewe ni mtoto au mfanyakazi mwenzie tu, huna la kumwambia.
Sasa nimekaa sana nikawaza namfanyaje huyu kijana, ni mdogo tu around 23 years (maana ndivyo wadogo zetu wa leo hujiona, kwamba ni watoto).

Nimeshafanya juhudi sana za kujaribu kumsaidia nijue anashindwa wapi kufanya kaz akapata wateja, nampa maelezo na maelezo na maelezo lakin wapi.

Nilipoona labda maelezo hayatoshi nikaamua kufanya kwa vitendo ili aone kwamba haya ninayomueleza sio tu naongea toka hewan, yanafanyika ndio maana namsisitiza afanye hivyo.

Nikawa natenga siku 3 kila week naingia sokoni kufanya marketing, mpaka mwez unaisha mimi nikifeli sana naimgiza wateja wawil lakin huwa namba inasoma mpaka 3 au 4 sometimes. Yeye hana anacholeta ofisin zaid ya stori na maelezo.

Nikaona bado labda message yangu hajaipata vizuri, nikabadil utaratibu, badala ya kwenda sokoni /marketing kivyangu na yeye kivyake ,nikaamua kwamba acha tushiriki pamoja. So nika mwambia kila unapokwenda kwa mteja wako kama una meeting, nijulishe twende pamoja.

Lengo hapa nilitaka kujua na kuona, ana engage vipi, nijue pa kumrekebisha, na pia nikataka nimfanya ANIONE MIMI the way na engage na hao hao watu wake ili ajifunze.

Mwisho wa siku nikienda nae marketimg, tunapata sales na tukirud ofisn naendelea kumpa shule na mambo mengine ili ajue namna ya ku improve.

UKUMBUKE HAPO MIMI SIO SALES PERSON BY PROFFESION, am purely a technical person. ni mtaa tu na harakat za ujasriamali zinanibidiisha kujifunza mambo mengi nisije kufa njaa.

Wakuu, nimefanya yooooote hayo lakin wapi!!!! Bila bila Na kitu kinacho ni irritate zaidi ni lack of morals kwake, hiv sasa naona hali inazid kuwa mbaya, kijana hana heshima kabisa.

Ujue mimi kama mtu ambaye nilishafanya ajira pia huwa najaribu kumtazama kijana kama mdogo angu ambaye anatafuta maisha na hili hunifanya kusita kuchukua hatua za haraka kimaamuzi nikiwa namatumain huemda ata change ila wapi!!.

IKabid niende hatua ya mbali zaid kwa kuongea nae kibiashara zaidi. Hii siku nikamuita nje ya ofisi.
  • Nikamueleza ni muda kiasi gani yupo hapa ofisin kwangu
  • Nikamkumbusha ni mshahara kias gani namlipa
  • Nikamuonyesha record za ni gharama kiasi gani ambazo nazi invest kwake katika masuala ya kazi nje ya mshahara.
  • Nikamuonyesha statements za bank ni jinsi gani income yetu as a companya ima flow
  • Nikamuuliza kwa hii comparison mdogo angu umafikiri hii pesa nayolulopa kama salary na marketing transport na ofisin unakula lunch na internet za bure, UNADHAN HIZ COSTS mimi nazi recover vipi kama wewe huna unachoingiza katika mzunguko? HANA MAJIBU.
Nikafikiri baada ya hii discussion ndefu sana labda anaweza pata akil atabadilika, WAAAAPI!

Wakuu huyu dogo sio ndugu yangu, sio jirani yangu, simjui hata ndugu yake mmoja, hapa tuko kikazi tu.

Nisaidieni, kwa haya yooote nimefanya, kuna kipi ambacho sijatimiza wajibu?

UNAWEZA KUJIULIZA KWANINI NIMEFANYA YOOTE HAYA?

Jibu ni simple kabisa, HIKI NDICHO NILIFANYIWA PIA japo mimi sikufika mbali hiv. Ajira yangu baada ya kutoka chuo, nilikua sijui chochote kuhusu kazi. Nakumbuka boss wangu ali dedicate sana muda wake kujifunza kuhsu kaz na majukumu maana hata mimi nilianza kufanya kazi kwenye kampuni ikiwa ndogo sana mpka inakua kubwa kufikia hatua ya kufanya total project sum ya 1B kwa mwaka by that time, toka 150M total project kwa mwaka wakati mimi ndio naingia hapo ofisin, kampuni ikiwa na boss na muhasibu tu.

Boss ndio kila kitu. So nilipoingia mimi cheap labour na degree yangu, boss alinifundisha sana sana sana kaz kwa moyo ili nimpunguzie majukum. That was 2014. Tofauti yangu na huyu dogo ni kwamba, nilikua nazingatia sana mafunzo.

Sasa hii ndio imenifanya kumvumilia kipindi hiki chote lakin kwasasa wakuu nahisi nimefika tamati.

Kwakua yuko kwenye mfungo wa Ramadhani, nime plan nitamuacha mpaka mwez wa Ramadhani uishe kisha nitam expell,

Nitamuondoa kazini, kuangalia namna nyingine.

Nakaribisha ushauri.

Wasalaam.
Hujafika hiyo hatua ya kuitwa Tajiri. Sema Waajiri kuonekana..... Mpe onyo kwa barua, mpe target akishindwa mwache siyo baba yako huyo.
 
Inasikitisha sana kaka. Tunawasaidiaje sasa?
Moral depravity ni kubwa..

Watoto wanalelewa bila utaratibu hakuna link ya wazazi kwenda kwa mtoto ndio maana mtoto anashindwa kujua akiwa kwenye kundi la vijana wenzie na anavyo behave sio sawa na akiwa katika meza na wakubwa zake.

Kimsingi ukichukua kijana wa miaka 23 ya enzi hizi hawezi kufanya maamuzi tuliyoweza kufanya enzi zetu, kijana wa 23 alikua amepevuka na almost anaweza kujisimamia.

Kuna dogo mmoja ana 25 aliniambia anataka kuja huku afanye process gani nilivyomuelekeza akajibu " kwani hakuna mtu anaweza kufanya process zote ikabaki mimi kuja tu"?

Yaani uvivu pia umewajaa , pita mtaani tu huko leo uliza vijana wa 20's mwaka tangu uanze wameshasoma andiko gani lolote hata kurasa 4 wakalimaliza utajua.

Au wape article ya gazeti wasome tu baada ya saa 2 waombe summary na uchambuzi wa key points kwa walichosoma utagundua kitu.
 
Back
Top Bottom