Nafikiri hii ndiyo sababu ya matajiri kuitwa katili wasiyo na utu

Kwa malipo haya mkuu,nadhani wale wanaotembeza mabeseni wakiona watajisikia vibaya sana.

Fikiria mtu anazurula 50kms na ili alipwe kwa mwezi ni mpaka mzigi wote uwe unakwisha.😀😀😀

Sorry labda dogo kuna namna nyingine anakufaa hujatuandikia hapa.
 
Lugha kali ndo utakayoelewa kirahisi. Mimi sio Mtakatifu Mathayo kwamba niongee kwa lugha ya kubembeleza. Punguza hizo mambo za professionalism. Nenda jinsi watu wanavyotaka. Inawezekana hata kazi nzuri unazikosa kwa kuendekeza huo utumwa wa professionalism huku ukipuuza codes muhimu za kitaa. Decision makers wa hizi taasisi za kibongo wana lugha zao za kipekee kaa chini ujifunze. Unavyosema una udhaifu kwenye management jua kabisa anguko lako haliko mbali endapo hutabadilika. Saa nyingine FUMANIZI HUIMARISHA PENZI. Punguza huo utakatifu uchwara. Huyo dogo kata maslahi yake yote mwachie nauli na lunch tu. Kama HAWEZI FUKUZA WEKA MWINGINE.
 
Hili nitalifanyia kazi kamanda
 
Madogo wengi hawajitambui...nilikuwa nao mimi wawili ofisini kwangu, nilianza na mmoja wakati namwajiri alikuwa peke yake alikuwa akifanya vzr sana nikaona kama ana overwork( kosa hili) nikamwambia amlete mwenzie wawe wawili daaah kilichonikuta sasa....kwanza wakawa na kiburi kwangu hadi watejaa....wakaanza nipiga kwenye mahesabu nikiwauliza wanasema hawajui pesa zinavyopotea...mwisho wakanipiga loss....hapo ndipo akili iliponikaa na kuwapiga chini...usicheke na nyani kwenye pale unapopatia ugali hawana maana binadamu.
 
Nilikuwa na akili kama za kwako mpaka nilipokutana na huu msemo “Siku Simba akimuonea huruma Swala, ndiyo siku atakufa njaa”

Kumfundisha kazi mtu ni muhimu sana maana hakuna aliyezaliwa anajua, lakin lazima umfundishe mtu anayeipenda kazi yake, mwenye nidhamu na anayeweza kuijua mipaka yake

Zingatia KUIPENDA KAZI
 
Nimekusoma chief.
 
Una uhakika huyu dogo Huwa anaenda marketing atakuwa akishachukua buku 7 anarudi gheto kulala
 
Nimesoma post nzima nimebaki kushangaa.

Hivi hawa generation Z wanaweza hasa kitu gani ?

Maana naona maturity kwa generation yao inapungua sana..

Miaka ile in our early 20's tulikua wanaume kabisa na wenye uwezo wa kuchanganua mambo na kufanya maamuzi mazito na kwa usahihi .

Nilipambana from the scratch hadi kutimkia majuu na kuanza moja ugenini bila kuwa na mtu hata 1 ninayemjua .

Leo hii mostly kws malalimiko nayoona kwa hawa generation Z na toddlers ni ndogo sana kwamba wao wanaweza kuongea, kutembea, kusoma na kuandika ila kimaamuzi naona kama bado sana.

Hawa vijana wa 20's naona wanaweza ngono, pombe, Tiktok, bangi , nk.
 
Inasikitisha sana kaka. Tunawasaidiaje sasa?
 
Hujafika hiyo hatua ya kuitwa Tajiri. Sema Waajiri kuonekana..... Mpe onyo kwa barua, mpe target akishindwa mwache siyo baba yako huyo.
 
Inasikitisha sana kaka. Tunawasaidiaje sasa?
Moral depravity ni kubwa..

Watoto wanalelewa bila utaratibu hakuna link ya wazazi kwenda kwa mtoto ndio maana mtoto anashindwa kujua akiwa kwenye kundi la vijana wenzie na anavyo behave sio sawa na akiwa katika meza na wakubwa zake.

Kimsingi ukichukua kijana wa miaka 23 ya enzi hizi hawezi kufanya maamuzi tuliyoweza kufanya enzi zetu, kijana wa 23 alikua amepevuka na almost anaweza kujisimamia.

Kuna dogo mmoja ana 25 aliniambia anataka kuja huku afanye process gani nilivyomuelekeza akajibu " kwani hakuna mtu anaweza kufanya process zote ikabaki mimi kuja tu"?

Yaani uvivu pia umewajaa , pita mtaani tu huko leo uliza vijana wa 20's mwaka tangu uanze wameshasoma andiko gani lolote hata kurasa 4 wakalimaliza utajua.

Au wape article ya gazeti wasome tu baada ya saa 2 waombe summary na uchambuzi wa key points kwa walichosoma utagundua kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…