Nafikiria kuachana na mke wangu

Nafikiria kuachana na mke wangu

Mwache huyo mwanamke haraka sana iwezekanavyo napia tafuta hela uwapime watoto DNA .

Mwanamke akishakuambia yupo mwingine anae msubiria amini nakuambia huyo siyo mkeo na hao watoto sio wako

Acha kukaza fuvu piga chini haraka iwezekanavyo
 
Shilingi ina upande wa pili, hapa umeeleza kwa upande wako na kawaida masuala ya ndoa shutuma kila upande huongeza sana chumvi.
 
Nikwambie tu Mtoa mada,
Ayo Maneno hujawahi tamkiwa peke yako,

Nishawai tamkiwa Sana hivyo na wife,
Enzi zile ndoa bado changa, tuna Mtoto 1

Kisha kesi ilipofika ukweni
Wakwe zangu wakatamka Tena,
This time ikiwa Ni msisitizo zaidi nimuache
Binti yao mrembo Sn, wakumuoa wengi sn.

Kikichotokea
Niliamua Kama unavyotaka kufanya,
maamuz yang hayakujali Nani ataumia
Nilijikuta nmeumiza Hadi wasiohusika,

Mwisho wa siku
mke na wakwe waliomba msamaha walikurupuka, Na maisha yaliendelea.

Uzi wa icho kisa,
umo humu MMU, nishawai kuuleta

Kaupitie
Unaweza kuokota mawili matatu[emoji1431]
Kwenye ule uzi ulidondoka fresh,niliokota mawe ya kutosha kupasua kabisa akili mbovu za wake wajinga wapenda mali
 
Kama Unachosema Ni Kweli, Na Hasa Hilo Neno Ukimwacha Yupo Mtu Basi Amejupanga Kuvunja Unyumba Mchana Kweupe Hadharani
 
Haya maneno ya kawaida ya wanawake.
Wakishaachika michepuko nayo ula Kona
 
Kuna jambo nimemwekeza alifanye vile mimi nataka Kwa kiburi kasema yeye hatofanya,pia kwenye maongezi yake nimesikia akisema nikimwacha Kuna mtu yupo anasubiri hiyo bahati Kwa hamu.

Pengine nafikiria nikiwa huru peke yangu nitafurahia maisha zaidi ijapokuwa nishamzalisha watoto ila naona Kwa huyu mwanamke siwezi kufanya milango yoyote ya maana Kwa kuwa naona tunatofautiana iq sana kiasi kuwa nilikuwa namvumilia hata akiniweka kwenye hasara.

Kimsingi sitaoa tena nitaishi maisha yangu lonely.
Pole,

1: Hapa tatizo ni EGO, umimi mwingi. Badala ya kushughulikia matatizo, mnajishughulika nyinyi binafsi.

2: Hata wewe ukifanya inner thinking/ kujitafakari, kuna uliyofanya kama binadamu kinyume na matarajio ya mwenzio. Ila kwa kuwa ni wewe na mengine yako ndani kwako unayarahisisha.

3: Hapa unaeleza ya mwezako, lakini huonyeshi yako pia.

4: Jinsi unavyo-address/ mzungumzia mwenzio pia ni tatizo. Umemzalisha vs mmejaliwa kupata watoto/family vs togetherness vs value.

5: Thamani ya familia yako vs ubinafsi. Umewafikiria watoto na hatima yao?

5: Kaa chini shusha pumzi/relax, fanya maamzi ukiwa very relaxed.

6: Je kwa umti wako hizi ndo busara za mwisho muumba kakuwewesha kwa umri ulionao?

7: Je maisha na mitihani ya jamii inayokuzunguks pia utaitupa na kuitotoka. Huwezi tatua tstizo kwa kulikimbia.

"Marriage is not a dot, but a life long learning process. Absconding is not a solution but your just enter a new school with its dos and don't."

Kucha zikikua, hatukati vidole bali tunakata kucha.

Maamzi mema.
 
wadau wa kataa ndoa tunaomba mtupokee..changamoto za ndoa zimetushinda rasmi
 
Kwa jibu hilo alilokupa, "kuna mwenzako ananisubiri", mkuu hapo hakuna kitu. Inaonekana yupo kwako kama vile yupo kituo cha daladala akisubiri usafiri, kwamba muda wowote gari ikifika anaondoka.

Sasa mimi nakushauri hivi; kama watoto wako ni wakubwa kiasi, tafuta hata dada wa kazi aje kuwalea (lakini asigeuke kuwa mke). Au la, kama una uwezo, wapeleke hao watoto shule ya boarding, halafu huyo mwanamke piga chini.

Huyo mkeo ana dharau na kebei, na usipoangalia anaweza kukudhuru endapo kutatokea ugonvi baina yenu mkiwa bado pamoja. Mwanamke mwenye staha kwa mmewe hawezi kusema maneno hayo.
 
"Kuna mwenzako ananisubiri" ukimuacha "hakuna Mwanamke utakayempata kama Mimi utanikumbuka" baada ya miezi kadhaa "Mume wangu nisamehe naomba turudiane yule alikua Shetani"
 
Kuna jambo nimemwekeza alifanye vile mimi nataka Kwa kiburi kasema yeye hatofanya,pia kwenye maongezi yake nimesikia akisema nikimwacha Kuna mtu yupo anasubiri hiyo bahati Kwa hamu.

Pengine nafikiria nikiwa huru peke yangu nitafurahia maisha zaidi ijapokuwa nishamzalisha watoto ila naona Kwa huyu mwanamke siwezi kufanya milango yoyote ya maana Kwa kuwa naona tunatofautiana iq sana kiasi kuwa nilikuwa namvumilia hata akiniweka kwenye hasara.

Kimsingi sitaoa tena nitaishi maisha yangu lonely.
Wazo baya kbsa utakuwa masikini vumilia tu yatakaa sawa
 
Mkuu umenichekesha sana, umewaza nini? Mimi siwezi kumuacha huyu mama...thiwezi asee!
😅😅😅 za kuambiwa changanya na thakooo... hii ndio Jf . Sema kuachana mzee hizi ndoa zetu ni kazi sana labda uwe bandindu maana waza upande wenu na upande na mashahidi inabidi uwe na sababu nzitoo sanaaa.. ukweli nilishatafakari ilia kila nikiwa unamuachaje mzee unakosa kifungu kisheria.. labda nimkimbie tu nikazamie na ulayaa hukooo
 
😅😅😅 za kuambiwa changanya na thakooo... hii ndio Jf . Sema kuachana mzee hizi ndoa zetu ni kazi sana labda uwe bandindu maana waza upande wenu na upande na mashahidi inabidi uwe na sababu nzitoo sanaaa.. ukweli nilishatafakari ilia kila nikiwa unamuachaje mzee unakosa kifungu kisheria.. labda nimkimbie tu nikazamie na ulayaa hukooo
Usiwaze kumuacha kama ni kwa makosa madogo madogo yanayovumilika, kosa kubwa ni moja tu, akiwekwa nje..hilo halina mjadala na yoyote.
 
Usiwaze kumuacha kama ni kwa makosa madogo madogo yanayovumilika, kosa kubwa ni moja tu, akiwekwa nje..hilo halina mjadala na yoyote.
mke wangu anampenda kinoma pastor wake kuliko mie nahisii.. nahisi hata heshimaa nyingii kwa pastor 😅😅😅 sasa huu si msalaa
 
Fanya hivyo tuwa huo mzigo wenzio wa nawaza wake zao wawaweke mazezeta ww mwanamke unawaza akutie hasara chukua hiyo chance MFANYE awe ndocha kama ndocha la kihindi halafu fungua duka unakuwa unaingiza mihela mingi zen unahamia kwa kajala na paula
Duh [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Una masihara sana mkuu😁😁😁 huna tofauti na mzab!
😅😅 kweli bro.. namuangali si unajua wengine hatusemagii tunakuwa tunasikilizia du.. kila saa anamuita daddy.. Unajua sie watu wazima unajua kabisa hapa navyopenda na anvayopendwa na kuheshimiwa mwamba tofautii. bora nikachukue kachakaramu kasiko na imani .. wanawake hawajui kuwa tuna wivu mkali kuliko wao sema sie tuna good management ya wivu wetu
 
Mnapondea sana wife, alichosema ni kweli na ukweli huuma.

Kwani akiachwa si ni kweli kuna mafisi mob wanangojea kujitwalia mzigo 😂

Ushauri wangu ni mdogo sana, kama mambo hazikai poa kwa boma mgawane fito, mambo za kukokota matatizo ni kupoteza muda.

Kama haeleweki jikate kula 50 kimbia nenda mbio, na kueleweka sikusudii hiyo kauli moja bali mjumuiko wa matatizo yenu yote.
 
Back
Top Bottom