Ninaloongelea hapa ni swala la kisheria. Si hadithi! Unajua nashangaa watu wanaponi attack. Mimi si Serikali kujibu yu wapi? Nachosema Lissu alitamka. Waziri Mkuu nae akatamka. Naamini maelezo yapi hapo? Nani yupo karibu na Rais? Kati ya Lissu na Waziri Mkuu? Tena akatupa salamu zake.
Swala Rais yuko wapi litajulikana mahakamani. Kwanini nimesema nitaishitaki serikali, na jeshi la Polisi? Unajua watu wakiona nimeandika nitamshitaki Lissu wanakimbilia kwa ushabiki kuanza kutukana. Hawasomi nilichoandika hadi mwisho. Siwezi kuweka hapa kila kitu, Ila katika madai yangu yatajitokeza mengi, ambayo yatahitaji majibu. Na kwa kupitia hii kesi itaweza pia kusaidia kujua Rais yuko wapi?
Ila watu hawelewi wamejaa ushabiki ulio na upofu. Its a very technical issue ukisoma madai.
Ila watu kutokuwa na uelewa hawajui chochote wamekalia umuwezi lisu na kadharika. Ila kwa watu ambao ni makini na wanasheria watakuwa wamenielewa. Ndo kesi zingine uwezesha kutungwa kwa sheria mpya, au kuondolewa kwa sheria iliyopo. Kutokana na maamuzi yaliyofikiwa na jaji. Ili swala litazamwe kisheria zaidi si kiushabiki.
Mfano, katika kuishitaki serikali; Serikali inazuia utoaji wa habari usizokuwa na uhakika nazo. OK, Kwanin hili swala la Rais serikali imekaa kimya? Na kuacha habari zienee. Uoni kuwa serikali kwa namna nyingine ndo imechochea uvumi kuenea zaidi? Nini majukumu ya serikali? Kama inazuia usambazaji wa habari basi iwe makini kutoa habari ambazo jamii itaridhika nazo. Hasa kuhusiana na afya ya Rais.
Katika kuishitaki serikali nitaomba Mahakama kuiamuru serikali itangaze juu ya afya ya Rais. Ili kuondoa sintofahamu katika jamii. Na si hivyo tu bali Rais ajitokeze wazi walau atoe salamu live kama kweli yu mzima si mgonjwa. Make wamekana kusema hata kama ni mgonjwa.
Hivyo sifungui kesi kupata fedha wala umaarufu. Nafungua kesi ili tujue ukweli ni upi.
Nimekuwa muwazi kwako kutoa maelezo kwakua umeuliza kiustaarabu. Wengi hawelewi lengo la yale niliyoyaongelea. Wakisoma tu Lissu mizuka inapanda bila kujua naongelea nini? Wakati nimesema nashitaki serikali hadi polisi.