Nafikiria kumpiga chini huyu Mwanamke, hajui kuishi kwa bajeti

Mkuu nakuelewa sana,binafsi sipendi pia mtumiaji wa hovyo
Budget ni kila kitu kwenye maisha
Huyo wako inawezekana ndivyo alivyolelewa ama ni wewe umemuonesha unazo za kutumia namna hiyo

Cha kufanya endelea kumuelekeza kuhusu umuhimu wa budget,mwambie hupendezwi na matumizi yake

Kama ataendelea kukaza fuvu unaweza kuchukua maamuzi magumu
 
😀😀😁😁😆😆😆🤣🤣🤣 Kisa kilo ya nyama 🙄🙄🙄😲😲😲😲??,nyie 😲😲 kwel kuwa uyaone siyo magorofa,mambo yenyewe ndio hayaaaa 🤔🤔🤔
 
Mahusiano yamekuwa rahisi sana siku hizi,watu hawana kuvumiliana,ndio sababu ndoa nyingi zinakufa kijinga. Jambo rahisi namna hiyo la kuzungumza ndio unataka kumrudisha mtu kwao?
kwangu mambo ya matumizi yanagusa hatima yangu ya bdae siyachukulii kiraisi kiongoz na huu ni mfano mmojawapo tu
 
Uwe unanunua nusu kilo ili ufungiwe kwenye gazeti la michezo maana unaleta mchezo na nyama wewe.
Idea nzuri. Badala ya kupeleka kilo moja we peleka nusu au robo kabisa.

Tatizo akiona nyingi anajisahau inaelekea. Ila ikiwa chache ata balance.

Nakumbuka ata mi nilileta uzungu nikanunua vile vi azam embe vya mia 6 nikanunua katon lote vinakua 24 nikaweka kwenye friji. Aisee kwa siku kuvipiga tano hadi 6 kawaida. Havikumaliza week.

Nikajua kumbe mi natakiwa ninunue tu rejareja, level za kuweka kwenye friji vinywaji bado.
 
Nusu kilo ya nyama inakuwazisha hivi..!! Maana ingekuwa nusu kilo usingelalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…