Nafunguaje NGO na kupata hela za mradi?

Acha utoto wewe. Kuna NGOs za MFUKONI kibao na zinapiga mpunga mwingi tu kila mwaka. Wafadhili wako MAMILIONI, kazi yako wewe ni kujieleza tu unataka kufanya nini na kwa gharama gani au kulingana na gharama zilizopangwa na mfadhili husika.
Unamiliki NGO mkuu?. Unajua Marais na wake zao wote wana NGO?. Unajua fund mnaomba kwa CV na competition?. Unajua USAID wanafund kwa namna Gani?. Unafaham pepfar wanafund vip?. Hiv unajua NGO ikiwa na miaka 5 bado changa?

Unajua maana ya kufanya mradi? Unajua miradi iliyowahi kufanikiwa resource mobilization ilikuaj?

Hayo unayosema wewe ni sentment. Sio rahis kama unavyotaka mkuu kama unabisha funguo NGO yako ili upate fund kma unavyotaka.
 
Mwenye wazo la kuanzisha NGO uko sahihi, anza sasa lakini itakubidi uombe funds kwa kuandika proposals. Huko nje kuna watu wana pesa nyingi sana, kazi yako wewe ni kujieleza tu...
Hakuna aliezuiwa kifungua NGO mana hata mm nategemea kufungua yangu next years.

Ngo nyingi changa zinaajiri vijana ambao ni cheap lakin hawana uwezo. MDH ya jamaa anaitwa Sando hata Instagram yupo. Mtaften anawez kuwapa ABC
 
Mkuu Inaoneka uko vizuri sana wengine hizo ndio ndoto zetu ..wachanga katika hayo mambo tunayamani tufike katika level za hao kina flaviana matata wanafanya vizuri ila tutafukaje pale?nani wamkutushika mkono kutuelekeza nn tufanye wapi tufike tufike pale binafsi natamani kujua vitu ulivoongelea hapo ntakuwa nmegain kitu kikubwa sana msada wako tafadhali mkuu toa shule kidogo hapo tusijeweka vyeti vyabusajili kabatini hii piano ni sadaka kama hutojali lkn na kwa faida ya wengine wenye nia
 
Unatakiwa kulipia mi nakufundisha hatua zote Hadi platforms wanazotumia kuweka katiba na cheti cha iyo NGO Hadi wazungu unawaletaje Tanzania na kuja kuvolunteer kwenye taasisi Yako na kutoa pesa kukusaidia kwenye miradi yako
Tusaidie kwa hapa tupe shule kidogo mkuu
 
Mkuu kwa mtazamo wako vipi operation zao umezionaje kwa hizo NGo tajwa?
 
Mkuu nafikiri kwa manufaa ya wengi fanya hivyo naamini hutakuwa umepoteza nguvu bure na utayaona matunda yake nahakika ndg, fikiria hilo
 
Hakika mkuu wewe unatoa mwanga na uelekeo na ninafikiri uko na mchango mkubwa sana kwa jamii yako, hongera kwa moyo wako wa kutoa dara bure hapa kwa manufaa ya wengi Mungu akubariki sana ndg
 
Ngoja niktulia nitaandka ninayoyajua
 
Kwenye kuunda NGO kuna kama vitu 3 .
1. Project proposal yenyewe.
2. Process za usajili wa NGO.
3. Ku get funds

1.Project proposal yenyewe .

Jitahidi kuwa specific kwenye topic, focus on problems and it's solutions.

Mfano:
1.Nishati mbadala
Unakuja na mkaa unaotokana na kinyesi cha Wanyama, ambapo process ya kutengeneza mkaa ni nafuu na salama kiafya na mazingira,pia bei yake ni nafuu ukilinganisha na mkaa wa kawaida katika ujazo sawa.

1.Panya road.
Unaangalia tatizo ni Nini,
utoro mashuleni,
Shule kutokuwa na mazingira mazuri ya kufundishia,
familia kushindwa kufuatilia maendeleo ya watoto Wao,
utumiaji wa madawa ya kulevya mashuleni.
mmomonyoko wa maadili Katika jamii.
ndoa AU familia kuvunjika
sabàbu bado zikaendelea etc.

Lakin wewe utafanya analysis yako kuangalia sababu 1,2,3 zisiwe nyingi ( coz , , gharama zitakuwa kubwa) ambazo utakazo kuja na suluhisho lake.

1. utoro mashuleni
2. utumiaji wa madawa ya kulevya mashuleni,

Lakin pia unaweza ukadili ña #2 Tu coz #1. Inasababishwa na #2. asilimia Zaidi ya 90% ya panya road wanatumia drugs.

so #2. Ndio inakuwa scope yako ya project.

Kwa wale walisoma degree kuandika project proposal watakuwa wanakumbuka.
NGO haina tofauti na project proposal

ukifanya hivi itakusaidia wewe kuendesha NGO coz bado wewe ni mchanga, nahata ukihitaji funds inakuwa rahisi coz mission yako ni 1 target only.

lazima Uwe na knowledge ya computer, words, excel, power point, access, outlook, E-mail,zoom. Cloud Drive.

Jitahidi ujue English vizur.

Uwe na laptop na internet ya kasi na uwakika pindi utakapohitajika kufanya mawasiliano.

jitahidi kuwa smart kuanzia kufikiri mpaka muonekano wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…