Nafunguaje NGO na kupata hela za mradi?

Asante sana
 
Yes, namiliki NGO na nimeshapewa grants na hao PEPFAR taasisi yangu ikiwa mpya kabisa. Miradi haitolewi kwa CVs, acha kupotosha watu wewe.

PEPFAR na wafadhili wengineo kwa kawaida wanatoa CALL FOR PROPOSALS, na kila mhitaji anaomba na wenye sifa wanapewa ruzuku (funds).

Hiyo Notice of funding ya PEPFAR - June 30, 2023 (nimeambatanisha hapo chini) kuna sehemu imetaja muombaji awe na CV? Punguza ujuaji ndugu
 

Attachments

Ngoja niktulia nitaandka ninayoyajua
Hujui kitu wewe. Balozi ya Japan inatoa funds kwa NGOs kwaajili ya miradi ya ujenzi; Ubalozi wa Finland unatoa funds kwaajili ya ustawi wa jamii; Kuna balozi za Canada, US Embassy, German, Australia, New Zealand, Poland n.k

Pia kuna UNDP, USADF, NORAD, USAID na wengine kibao, wote hao wanatoa funds kila mwaka na NGO yangu ni mnufaika mkubwa sana huko. Hakuna kutuma CV, kazi yako wewe NI KUJIELEZA TU wanapotoa CALLS za proposals zao
 

Attachments

USAID Tanzania wana hii call for papers (concepts), maalum kwaajili ya local NGOs. Ni fursa kwa NGOs zote, kazi yako wewe NI KUJIELEZA TU; unataka kufanya nini? na utafanyaje? kulingana na maeneo ya kufanyiwa kazi ambayo wameyaainisha kwenye "addendum" husika.

NGOs ndio sekta pekee ya uhakika kwa vijana wa kitanzania kuweza kujiajiri. Hata kama NGO yako imesajiliwa LEO HII USIOGOPE, anza sasa. Kuna wafadhili MAMILIONI, tafuta na andikia proposal
 

Attachments

Asante mkuu Kwa maelezo haya
 
Asante mkuu Kwa kututoa tongotongo
 
Najaribu kuelewa ulivyosema tunaanzia suluhu kulifuata tatizo lakini naona pia mfano wako na wa jiwe angavu unafanana.

Yeye ameona tatizo la panya road wewe umeona ukatili na wote mkaimagine suluhu.

Bado nataka kujifunza hii approach yako
 
Najaribu kuelewa ulivyosema tunaanzia suluhu kulifuata tatizo lakini naona pia mfano wako na wa jiwe angavu unafanana.

Yeye ameona tatizo la panya road wewe umeona ukatili na wote mkaimagine suluhu.

Bado nataka kujifunza hii approach yako
Tatizo a jamii moja Lina sababishwa na vitu vingi sana. Hapo kwa panya road Kuna sababu nyingine ni pasua kichwa.. zilitakiwa kuwa preventive sio responsive.

Kama panya road ni vijana. Je ni wamgap walifikiwa na miradi ya vijana kama ile mikopo manispaa wakaiacha na kuingia huko?. Likishatokea tatizo mkakati hapo ni responsive na preventive. Mnazuia yasiotkee Tena na mnatatua lililopo.


Ukiangalia sababu za kuwepo kwa panya road.. moja utaikuta UKOSEFU WA AJIRA. JE utawaajiri?

Cc. jiwe angavu
 
Tuma picha ya kazi zako hapa tuone kama kweli unanufaik na concept paper tu. Mambo yamebadilika sana wakuu Kuna mradi umefungiwa naufaham pale mikochen na hela zilishatolewa. Watu walikuwa wananunua kesi.. siku hiz Kuna micro management.

Fund ya USAID kwa mwaka ni mwezi wa pili. Na waliyepata mwaka huu wanajulikana. Wew imepata fund kwa call Gani?
 
Hiyo fomu ya USAID mwaka Jana mm nimejaza mwemyew na inataka mjaze majina ya watu watatu na uwezo wao na wanaakt kama nani hapo kwenye NGO.

Pepfar uliweka Nini na Nini wakati unaomba fund?
 
Mkuu,Kama kitu hujui usiseme hakuna,bali sema Sijui.Hata hizo Giant NGO nazo zilipitia njia hizo hizo....Kama NGO yenu ina 10 years na bado hamjawa na stable financing basi shida ni ninyi na sio NGO wala mifumo ya NGO ila kwa kauli yako hapo ina maana hamko innovative mnafikiri tu PESA mtpewa kwa sababu mna cheti
 

Fundraising ni competition. Call for Proposal zinatolewandani ya muda maalum kwa mwaka sio uandike tu upeleke upewe hela. Unless kama una target na Mabenki. Nadhani unatishiwa na huyu member anaekosoa hapo juu. Right?
 

Panya Road wengi kwa umri wao ni umri wa kua shule so ajira inaweza ikawekwa kando.

Ok so approach ikiwa preventive inakua na mashiko kuliko ikiwa responsive
 
Fundraising ni competition. Call for Proposal zinatolewandani ya muda maalum kwa mwaka sio uandike tu upeleke upewe hela. Unless kama una target na Mabenki. Nadhani unatishiwa na huyu member anaekosoa hapo juu. Right?
Hapana mkuu wala sijatishwa na mtu.Katika kutafuta Funds kuna Njia nyingi na hiyo ya ku respond to Calls for Proposal ni Moja na mara nyingi ni very competitive kwa sababu zinakuwa zinafanyika kwa mchujo,deadline ni fupi na pia kiasi cha pesa kinachotolewa kinakuwa ni fixed kikiwa ni lengo maalum.

Hata hivyo katika kufanya Fundraing kuna approaches nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia cha msingi ni kuhakikisha kwamba unakuwa na MIX nzuri ya Strategy na unafanya Networking ya kutosha na cha muhimu zaidi ni kuhakikisha kile ambacho unafanya una passion nacho.

Tatizo la NGO nyingi zilizofeli ni zile ambazo watu wanaanzisha bila kuwa na passion na kile wanachofanya.Wanaanzisha kwa sababu wanasikia au kuona NGO zinapata PESA wanafikiri ni RAHISI.Wasichokijua ni kwamba NGO industry ni BUSINESS kama BUSINESS nyingine na zina ushindani na changamoto za kila namna.Cha muhimu ni kuelewa Strategically ni nini unataka kufanya,kwa nini unataka kukifanya na zaidi ni kuhakikisha kwamba unafanya utafiti wa kina na kuwa tayari wakati wote kutumia fursa ambazo zinajitokeza.
 
Uliwahi kupeleka mradi fund mwezi gan nje ya ule nwez wa call for Proposal? Ulipata?. Kama ndio au hapana unajua kwa nn?

Maybe approach zako shea na sisi hapa. Au nitumie jina la ngo yako hapo juu tuje kukutembelea KESHO
 
Uliwahi kupeleka mradi fund mwezi gan nje ya ule nwez wa call for Proposal? Ulipata?. Kama ndio au hapana unajua kwa nn?

Maybe approach zako shea na sisi hapa. Au nitumie jina la ngo yako hapo juu tuje kukutembelea KESHO
Dah,Mkuu,so natakiwa nikupe Jina la NGO,Ofisi ilipo uje ututembelee Just to Prove a JF discussion to you?OK iko hivi kwanza SINA NGO yangu,I work with multiple NGOs.Pili hata kama ningekuwa na NGO sidhani kama ningeshare approaches zangu zote hapa JUST like that.

Ila kwa sababu ya kuelimishana nitakujulisha yafuatayo:

Kwanza kuna NGOs au TRUSTS ambazo zinajihusisha na kutafuta FUNDS kwa ajili ya NGOS.Yaani wenyewe wanatafut Donors na kusimamia Funds za Donor na kuzitolea Taarifa kwa Donors na wao wanachukua Taarifa kutoka kwa hiz Final CBOs na NGOs.

Pili kuna sector specific Funders ambao wao wanalenga Funding kwa ajili ya Sector fulani TU mfano,Afya tena with specific area,Education,Environment etc

Tatu kuna Corporate Donors ambao wengi wanaweza fall katika eneo la CSR and Philantropy.

Sasa ukitazama hapo utaona kwamba nje ya hizo Call for Proposal kuna POOL kubwa sana ya FUNDERS ambayo unaweza kuitumia cha muhimu ni kuhakikisha kuwa NGO yako ina STRATEGIC ALIGNMENT na TRACK RECORD nzuri itakayowezesha NGO yako kupata PESA.Kufikia hapo inahitaji JITIHADA zaidi ya KUSAJILI tu NGO.

Unahitaji KUJUA nini UNAFANYA na UNAKIFANYAJE.

Nafikiri kama uko makini kuna kitu umekipata hapa.
 

Naona nabishana na gugo. Anyway! Nakutumia address yangu ukipata nafass.. TUTEMBELEANE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…