Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Huyu hana akili tu ana gari lakini analia njaa na kusema amekata tamaa ?

Hivi anajua kukata tamaa huyu kweli?
 
Pole sana ndugu yangu;Binafsi nimekuja kuamini kuwa duniani marafiki ni wachache sana,pale nilipoamua kwenda kujiendeleza kielimu hivyo kujikuta ktk hali ngumu kiuchumi,ukimpigia mtu simu ya kuomba akukopeshe kiasi fulani cha pesa unakuta mtu anakupiga chenga hata simu hapokei,wakati huo nilipokuwa kazini nilikuwa nikimsaidia.Aisee binadamu mwone km alivyo.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu usiseme hivyo,tumia lugha nzuri kumshauri mwenzako kuwa afanye nini kwa kutumia gari hiyo aliyonayo?.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
Nyenzo anazo halafu analia njaa ??

Unamshauri nini mtu wa hivi ?

Auze na hiyo gari ya tatu apate hela ya kulipa kodi ili ikiisha afukuzwe akaishi mtaani ajifunze maisha ya mtaa.
 
mkuu watu wengi wanapitia magumu..na hasa hii 2020 imekuja na mambo mengi sana..kaa tulia kichwa kiww cha baridi..badili mfumo wa maisha..anza moja..usiwafikirie marafiki na mke kea sasa...anza upya na anzia chini kwa kidogo unachopata...
usiishi katika majuto..hali kama yako ilinikumba 2015 nilituliza kichwa ila pia mke hakuwa na wenge kama wako.kwa sasa tunasonga japo bado hatujafika tunapotaka...
Usiuze Nyumba..kwanza jifanye kama haipo...usiwaze kuiuza ...
 
Pole sana ndugu. Bahati mbaya sina cha kukusaidia kifedha. Ila nina jambo moja la msingi la kukushauri, kila jambo linalofanyika lazima bwana aruhusu. Na kwa kila analoliruhusu kuna sababu.

Amin nakuambia, baada ya kupita kwenye moto huu, ukiwa mvumilivu, utatoka mtu mwingine kabisa. Hutaamini muda huo ila ndio ukweli.

Shukuru Mungu umepata nafasi nzuri ya kuwajua watu muhimu kwako, ambao wapo tayari kusimama nawe. Wengi huwapa umuhimu wale ambao hawastahili.

Mtegemee Mungu pekee, atakuvusha.
Bwana Yesu akusaidie!
 
Wewe naye ni kilaza wa taifa kama umeshindwa kuelewa concern yangu,Mimi nimejaribu kuvaa viatu vya huyu bwana hiyo gharama ya kununua hayo magari matatu ni pesa ambayo ingetosha kumalizia nyumba aliyojenga na sasa angekuwa kwake ASINGEDHALILISHWA KIASI CHA KUTOLEWA VITU NJE ANGEKUWA AMESHAHAMIA KWAKE.Hili ni tatizo yaani wewe unafanya kazi kampuni binafsi unakimbilia kununua magari badala ya kukamilisha nyumba.HATA HIVYO HAYO NI MAWAZO YANGU USINIPANGIE CHA KUSHAURI PIMBI WEWE.
 
Pole ndugu,,, mungu ana makusudi yake jaribu kutambua funzo analokupa leo ili rizki yako ikirudi uwe imara has a katika kuwekeza nguvu zako kwa Mungu.

Nimeona mlikuwa n ujenzi wa nyumba je kwanini msiiuze uanze biashara? Au ukopee mkopo hiyo nyumba?
Itaisha tu. Aiache angalau itakuwa asset ambayo itamsaidia mbeleni. After all bei kwa sasa ziko chini sana na bado wanunuzi hamna!
 
Mbona kiumli bado mdogo halafu unataka kukataa tamaa, jichanganye kariakoo au mansense utakutana na watu wanaelimu ya maisha, ila kuwa makini usitapeliwa soma mchezo jiweke kalibu, baadaye uza gari kwa bei yoyote anza biashara. Jiwe alaaniwe ameharibu maisha ya watu wengi sana
 
Dah pole sana mkuu ukweli maisha yanashida sana na maisha ni milima na mabonde cna Cha kukusaidia Ila umenigusa sana mkuu Mungu atakuvusha tu naimani kaka utatoka wanawake ndivyo walivyo Ila vumilia na pambana kaka
 
Dah yaani mimi niko na matatizo yangu lakini baada ya kusoma hii mada nikajiona nina unafuu mkubwa sana.
Kweli nimeamini maisha ni kama filamu yaani kuna kupanda na kushuka.
Lakini kitu kingine pia kwa sisi wasomaji iwe kama funzo kwetu,japo sijajua mtoa mada alifanya kazi kwa miaka mingapi.
Lakini kitendo cha mtoa mada kununua magari mengi wakati mahali pa kulala hana hii ni mistake tayari.
Kwenye issue ya money savings simlaumu kwa sababu tayari alishakuwa na majukumu ya kulea familia na kusomesha.
Na lengo langu sio kukashifu au lawama coz hali anayoipitia kwa sasa binafsi imenigusa sana.
Pia mtoa mada nakuomba pm kama hutojali kuna magroup yetu ya kazi huwa tunapeana ushauri mbalimbali na kupeana taarifa za kazi.
 
Mkuu umeongea point kubwa sana.
Hapo mungu amempa majaribu tu apate kujifunza marafiki wa kweli ni akina nani na wanafki ni akina nani.
Imagine leo hii anapata msaada hadi kwa housegirl inamaanisha ukarimu wake ndio umemsaidia otherwise kama angemnyanyasa asingeupata msaada wake.
Hii hali iliwahi kunikuta aisee usiombe kabisa ikukute yaani utahisi kama dunia imepinduka.
 
Yani mwenyewe nimeshindwa kushangaa sema vijana wengi siku hizi tunapenda sifa na maonyesho sana ukijakushituka muda umekuacha siku nyingi.
 
Pole sana kwa hizo changamoto aisee mm naelewa sana nn maana ya kutengwa na kuonekana kama msumbufu, hakuna thamani Hasa na watu wako wa karibu kwasababu mm pia nishawahi kuwa katika hali hiyo, kubwa zaidi unahitaji utambue kuwa maisha Yamebadilika hivyo unatakiwa ubadilike pia kwa maana Sasa hv acha kumfikiria mkeo na wanaoa maana naamini wako salama huko walipo zaidi Kadri unavyozidi kujitetea kwake ndio unazidi kumpandisha hasira na kumuongezea chuki, pia kama unamiliki gari kubwa ambalo unaweza uza ukapata IST uza ili update hata gari ya kufanya Uber na utafute hata chumba cha bei rahisi kupanga maana hata Rafiki yako itafika muda atachoka sisi binadamu na utampoteza hata huyo, kama unaweza pia fanya hata kusafiri urudi nyumbani kama umeenda kusalimia hiyo itakusaidia zaidi naamini. Lakini ukitaka uendelee kuprovide kama zamani kwa Familia na ndugu utadhalilika zaidi kwasababu I know only few people really care about you ambao wako ready to fight along side u to the end nao ni wazazi tu. Naamini Mungu anakupa lesson ujue kind of woman uliekuwa nae ili hata ukirudi katika hali yako ujue Unaishi na mtu wa namna gani. NAKUOMBEA MUNGU AKUPITISHE HICHI KIPINDI SALAMA AISEE NIKIGUMU SANA MAANA EVEN ME I WAS ABOUT TO LOSE MY SOUL AND SELF KAMA ISINGEKUWA WAZEE, THIS PEOPLE WANAUJASIRI, UCHUNGU, LAKINI PIA BUSARA SANA FANYA UENDE HATA KUWASALIMIA
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…