Wataalam wa mambo... twende kazi....
Kwani huwa inachukua muda gani mtoto kuwa na rangi wa wazazi wake..? Au kufanana na wazazi wake hata mmoja tu.
Baba mweusi, mama mweusi lakini mtoto katoka mweupee. Ndiyo najua kuna ile rangi nyeupe ya kitoto lakini kama wazazi ni weusi baadae inabadilika na anakuwa mweusi, lakini mbona huyu rangi haibadiliki?
Mtoto ana miezi kumi saizi ila hata dalili za kubadilika rangi hamna, toto bado ni jeupee.
Nahisi kuna uwepo wa miso misondo hapa a.k.a kitu kizito sasa subiri.
Niliapa katika maisha yangu siji kuuwa mtu hata siku moja, kwanza ni zambi ila kumbe inawezekana kiurahisi tu aisee na wala sio zambi kumbe.
Ngoja kwanza muda wote najifanya kama sijashtuka vile nakaa na mtoto nacheza nae kumbe mjuba namkagua chalii na bado sijioni kabisaaaaa.
Tumefanana kitu kimoja tuu, ile mistari ya kwenye viganja... Alama zilivyojichora kwenye kiganja changu cha kushoto nayeye cha kushoto ziko vile vile.... Na za mkono wa kulia wangu zilivyojichora na yeye vile vile ila the rest ni utofauti wa kiwango cha lami....
Kuna time nikiwa nimempakata namcheki dogo weeee kama anakujaa alafu anakataaa..... Napiga funda Moja la safari... Namcheki tena weeee anakuja alafu anakataaaa.
Nahisi kuna siku nitatangazwa kwenye kile kipindi cha matukio ya wiki pale I.T.V kwa kitendo ambachi nimepanga kukifanya. We ngoja, time will tell.
Mkuu kama unayosema ndio kweli yapo akilini mwako, Pole sana! Ila kama ni changamsha kijiwe poa!
Nakusihii tuliza akili na ufanye yafutayo!
Kwanza amini fact kuwa inawezekana mtoto akawa wako au siyo wako!
Fact ya pili ambayo unapaswa kuikubali ni kuwa ama mtoto awe wako au siyo wako malaika hana hatia, hivyo hastahili kwa namna yoyote kupata adhabu ya direct au indirectly!
Aidha, jiweke wewe katika nafsi ya mtoto husika!
Pia elewa kuwa endapo utamfanyia tendo la ukatili mtoto au mama, utakuwa umefanya ukatili kwako mwenyewe, mtoto, jamii yako na muumba kama unaamini katika imani!
Suala la mashaka ama kumchunguza mtoto kama wako au siyo wako ni la kawaida kwa mwanaume na viumbe hai wengine wenye IQ, hivyo nawe una uhalali wa kufanya hivyo!
Endapo utajiridhisha kuwa siyo wako, tafadhari, kubali matokeo na fanya maamuzi mawili tu: samehe na endelea kumtambua kama wako na ikiwezekana endelea na mahusiano na mama watoto wako ingawa ni ngumu. Kuna mchungaji wa kisasa mjini yeye analea tu na anajuwa kuwa sio wake. Pili, copy option ya Yusuph dhidi Bikira Maria, mwache kimya kimya bila yeye kujua kwa faida ya mtoto. Ikiwezekana tafuta issue nyingine ya kuachana!
Nakusihi usione jambo la ajabu kuchapiwa na mkeo kuzaa mtoto wa nje bali fanya maamuzi ya kujilinda wewe, Ndugu zako na mtoto husika. Ukifanya vinginevyo unaweza ukajikatitli wewe, mtoto na kuisababiashia maumivu ya kudumu jamii yako.