Nahisi mshawahi kumuona Nelson Ntombela Raia wa Afrika Kusini kwenye mitandao ya kijamii?

Nahisi mshawahi kumuona Nelson Ntombela Raia wa Afrika Kusini kwenye mitandao ya kijamii?

Kwenye Rhythm City mara ya mwisho kuitazama alikua ni mhalifu wa siri ila alikua anamiliki Bar akiwa partner na mtu mwingine
 
Bila shaka umekutana sana na picha hii katika mitandao, mfahamu mhusika wa picha hiyo. Nelson ni mkazi wa Kagiso, Krugersdorp nje ya mji wa Johannesburg, amezaliwa April 6, 1987 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba..
Mnamsingizia, mbona haimaindi pochi ya mdada hapo kwenye siti! Au tayari kesha isachi ndiyo maana anacheeeka.
 
Hahahaha yani huyo Jamaa picha yake imeingiziwa manenoo mpaka raha
IMG-20210114-WA0000.jpg
IMG-20210111-WA0027.jpg
IMG-20210105-WA0026.jpg
 
JamiiForums ni kisima cha maarifa , ndiyo forum mtanzania anaweza pata taarifa za mambo meng anayohitaji Kwa lugha yake.... Huyu jamaa picha yake imetrend Sana hv karbuni kwenye social network ...napenda kumfahamu huyu mwamba ni Nani , inabd nimjue Tu mana kabeba kaption karbia Nyanja zote , kisiasa ,kimichezo , kielimu , kimapenzi , kihisia na hata kidini
FB_IMG_1610643184597.jpg
 
Jamii forum ni kisima cha maarifa , ndiyo forum mtanzania anaweza pata taarifa za mambo meng anayohitaji Kwa lugha yake.... Huyu jamaa picha yake imetrend Sana hv karbuni kwenye social network ...napenda kumfahamu huyu mwamba ni Nani , inabd nimjue Tu mana kabeba kaption karbia Nyanja zote , kisiasa ,kimichezo , kielimu , kimapenzi , kihisia na hata kidini
View attachment 1677594
Huyo ni mcheza movie wa huko kwa Madiba.
 
Ngoja nimuelezee huyu jamaa, kisa chake kina ya kujifunza.

Anaitwa Nelson ni mkazi wa Kagiso, Krugersdorp nje ya mji wa Johannesburg, amezaliwa April 6, 1987 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba.

Nelson amekulia katika mitaa ya wahuni, alikuwa mhuni pia wakati wa utoto mpaka akiwa mtu mzima, mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 tuu alifungwa katika gereza la watoto kwa makosa ya ukabaji wa kutumia silaha.

Hata akiwa gerezani aliendelea kuwa kiongozi wa makundi ya kihalifu yaliyokuwepo kwa Siri gerezani, alikutana na makundi mengine ya kihalifu na akawa kiongozi wao, na hata alipoachiwa miezi kadhaa mbeleni, mtaani kuliendelea kua chini ya utawala wa makundi yake kama kawaida, kiufupi alikuwa jambazi.

Nelson aliendelea na ujambazi kwa miaka mingi zaidi hali iliyopelekea mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 26 kukamatwa tena na kufungwa gerezani miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kubomoa nyumba na kupora mali.

Mwaka 2014 akiwa jela mama yake mzazi alifariki, likawa pigo kubwa sana kwake na hii ilimsaidia kujiapiza kua atachana kabisa na ujambazi na kuishi maisha ya amani atakaporudi uraiani.

Baada ya kutoka Jela akaanza kujihusisha na kuigiza filamu akitumia jina la Chicken, hili ni jina alilopewa na wanakijiji wa kule alikozaliwa kutokana na tabia yake ya wizi wa kuku wakati akiwa mdogo. Filamu yake ya kwanza kabisa inaitwa Rhythm City (series) iliyoanza kutoka mwaka 2007, yeye aliikutia mwaka 2017 ikiendelea.

Kutoka hapo Nelson alianza kuona mafanikio makubwa katika kuigiza filamu kwani aliendelea kuonekana katika filamu na TV shows nyingi kama Isidingo, Generations: The Legacy na Isithembiso.

Na hiyo picha ni katika harakati zake za kikazi akiwa location.
 
Back
Top Bottom