na madhara yake kiafya ni yapi?
Kukosa usingizi. Kinywa kutoa harufu mbaya, inaweza kuamsha vidonda vya tumbo, matumizi makubwa na yaliyopitiliza ya kahawa yanaongeza acid mwilini ambayo ndio huleta shida ya vidonda vya tumbo kama unavyo.
Kimsingi unatakiwa kuwa moderate kwenye matumizi ya kahawa sababu ni kinywaji ambacho kina umuhimu mwilini ila matumizi yake yanataka umakini na balance.
Kunywa maji kwa wingi ili ubalance. Tumia kahawa baada ya kupumzika vizuri yaani usitumie ukiwa katika hali ya kuchoka na haujapumzika. Kama una pressure ya kupanda kahawa haitafaa. Kama una pressure ya kushuka kahawa ni nzuri kwako.
Enjoy kikombe chako cha kahawa.
By the way mimi kahawa yangu ambayo napenda tumia ni Brand ya Nestle ile chupa yake ni ya kioo. Halafu ni ya chenga chenga kubwa yaani sio unga ule mlaini kama hii kahawa ya Africafe.
Huwa napenda kutumia maziwa fresh ya ng'ombe, ngamia au mbuzi yale mazito sana.
Kuiandaa huwa nachukua maji ya moto nachemsha natia kwenye chupa ya chai kwanza kwaajiri ya baadae.
Tumia maziwa fresh ya mnyama yoyote kati ya hao nimetaja. Maziwa fresh yakichemshwa huwa yanaweka utandu kwa juu wakati yanapoa kama cream nzito sana.
Huwa nauchota kwa kijiko kikubwa kile cha kuchotea mboga nauweka huo utandu kwenye chombo pembeni kwaajiri ya kuhifadhi kwenye friji. Ili upate huo utandu maziwa hakikisha maziwa yawe yale ambayo yana mafuta ambayo yanatokana na ng'ombe,mbuzi au ya ngamia wanaolishwa vizuri wanatoa maziwa yana unjano njano. Hayo maziwa ukichemsha yanatengeneza layer kubwa ya hii cream nzito.
Unachukua ile cream ya maziwa iliyo kwenye chombo unachanganya na maziwa ya unga unapiga kama vile unavyopiga yai kwenye kibakuli ili ijichanganye freshi.
Kisha unachukua kahawa unakadiria uhitaji wako. Mimi huwa natumia mug so huwa natumia kijiko kikubwa cha chakula (table spoon [emoji1633]) naweka viwili kwenye kikombe.
Naweka yale maji ya moto kidogo yaani kama ujazo wa kale kakikombe kadogo sana ka chupa ya mtoto ya uji. Naweka maji kidogo ya moto ili kuiyeyusha ile kahawa ila isiwe nyepesi sana sababu ya kikwekwa maji mengi. So unaweka kidogo hayo maji ila iwe nzito sana isiwe nyepesi utaharibu.
Kisha napasha ile cream kwenye moto kidogo tu iwe ya moto kisha naitoa. Namimina kwenye ule mchanganyiko wa kahawa na maji ya moto. Then natia sukari, mimi huwa natumia kijiko kikubwa kimoja na nusu cha sukari. Then nakoroga.
Inakuwa nzito mithiri ya mtindi so unakuwa ni cream coffee nzuri balaa. Hiyo huwa natumia sana weekends nikiwa nimemka baada ya kulala.