Nahisi nimekuwa mlevi wa Coffee, natamani kuacha

Nahisi nimekuwa mlevi wa Coffee, natamani kuacha

mkuu hutaki kuishi miaka mingi embu pitia hapa hivi. ..

BBC walishawai kuandika makala moja hivi kuwa wanywa kahawa huishi miaka mingi link hii hapa

Sasa ni kikombe kimoja kila siku 🥲🥲 mimi nakunywa zaidi ya vikombe vinne na ni lazima iwe very strong 🥹🥹
 
pia makala hii....



nimalize kwa kusemaa jaribu kutafuta replacement ya kahawaa.. yan upunguze kunywa kahawa uanze kula chocolate... kupunguza addiction
Ninaendelea kujaribu lakini ninashindwa.

Naweza sema leo nitakunywa peppermint tea tu lakini haipiti muda chap uchovu unanikunbuka ghafla naona kahawa ndio suluhisho 😔😔
 
Mwenye uraibu huwa akipishana na birika anapata kiu hata jua kali la saa 7 mchana umefikia hatua hiyo?
Bado sijaifikia hii hatua Lucha lakini nahisi nisipopata mbadala nitaelekea huko
 
jitahidi uache kabla mambo hayajaanza kuwa mengi japo si rahisi kama umezoea.

binafsi nataka niache kula vyakula vyenye mafuta kabisa na nipunguze kula wanga
Kuna comments nimezipitia hapa nitazifamyia kazi.

Unakula vyakula vyenye mafuta mengi au kidogo?

jitahidi ndugu yangu ingawa si kazi rahisi
 
na madhara yake kiafya ni yapi?
1683831811723.png
 
Mimi nilikuwa natengeneza viungo vya chai mwenyew Huwa naweka tangawiz na pilipil manga kidogo sahiz naona hali mbaya natumia pilipili manga nyingi na tangawiz kwenye chai Yani chai had iniwashe hasa ndo najielewa
Hiv Haina madhara kiafya?
Kwa ninavyojua having madhara….black pepper ni nzuri sana mwilini
 
Kuna comments nimezipitia hapa nitazifamyia kazi.

Unakula vyakula vyenye mafuta mengi au kidogo?

jitahidi ndugu yangu ingawa si kazi rahisi
nataka niache kabisa utaratibu wa mafuta nile mchemsho pure.
nitaweza maana nia ninayo
 
Unakunywa kiasi gani kwa siku au mara ngapi? Bila shaka wewe siyo mnywaji sugu kama unavyodhani. Kuna nchi inaitwa Finland nenda uone jinsi watu wanavyokunywa kahawa! Kuanzia asubuhi mpaka jioni kila siku. Tena siyo instant coffee bali ile iliyokaangwa na kusagwa. Na ni moja ya nchi zenye watu wanaoishi maisha marefu. Kwa ujumla ni kuwa kahawa haina madhara. Labda kama unachanganya na sukari nyingi! Jaribu kunywa kavukavu na utakuja kuona kahawa bila sukari ni nzuri kuliko yenye sukari.
Nakunywa zaidi ya mara nne Kwa siku.

Yap nakunywa na sukari lakini pinch of it..

Labda decaffeinated coffee mkuu
 
Sijawahi kusikia kuwa vina madhara, tangawizi au pilipili manga. Zaidi nimesikia wanasema ni vizuri kwa afya. Ni Bongo tu pilipili manga haitumiki kwa wingi lakini nchi za Asia na hata Ulaya, pilipili manga inatumika sana kwenye kupikia na ku-marinate nyama.
Kabisaa
 
Back
Top Bottom