Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

i think wewe ni pacha wangu kabisa, 🤣🤣🤣🤣🤣🤣

nimefanya kazi ya ulinzi for 5 years kampuni 3, China security ile inayo linda mwendo kasi...!

Gardaworld na Ws insights... baadae nikaamua tu nijiajili as a bodaboda driver 🥲🤣🥲🤣
 
Kaokoke wewe Fala! Mnaambiwa mkimbilie Yesu mnakataa! Unadhani huko uendako ndo kuna unafuu? Utaishia kuzimu motoni! Tafuta kanisa la walokole wakuombee na uokoke! Fala wewe! Eti mnamkataa Yesu! Ona sasa!
 
Duh we balaa!nimesurrender mkuu
 
shukrani sana mkuu.. pikipiki naijua sema self esteem is so down ndio maana nawaza labda niende shamba nikaji isolate labda kidogo
 
Kaokoke wewe Fala! Mnaambiwa mkimbilie Yesu mnakataa! Unadhani huko uendako ndo kuna unafuu? Utaishia kuzimu motoni! Tafuta kanisa la walokole wakuombee na uokoke! Fala wewe! Eti mnamkataa Yesu! Ona sasa!
Huu uandishi wako,hauleti maana ya unachokiandika!na unamuaibisha huyo Yesu mwenyewe.
 
😒😒😒
 
Meditation ina clear hivyo vitu vyote na Inakupa Nguvu na kujiamini sana..

Sasa kama utashindwa kumpata min -me mpaka wiki hii ikiisha utanishtua
 
hongera sana Rafiki yangu... uliwezaje...!
Labda nikupe story yangu kwa ufupi...
1. Baba alikua mume wa mtu.
2. Mama akanusurika kuuawa mimi nikiwa tumboni.
3. Mama na mimi tukanusurika kufa wakati nazaliwa.
4. Nikaungua na moto nikiwa na mwaka mmoja nikanusurika kua kipofu.
5. Baba anatutelekeza kabisa nikiwa na mwaka mmoja, huku nikiwa simjui ndugu yeyote upande wa baba.
6. Ndugu wamama wananichukia kiasi cha kunitengenezea kesi hatari polisi.
7. Namaliza form 4 bi mkubwa anakumbwa na ugonjwa nashindwa kuendelea na masomo.
6. Nikapata kazi nikajisomesha kwa taabu.
7. Nikiwa na uhakika wa kufaulu mtihani matokeo yanatoka nimefeli form six.
8. Kila nikipambana nijiendeleze kielimu yanazuka majanga mara nyumba inuziliwa na mafurika inabomoka au kazi naachishwa/naacha
9. Napendwa na mwanamke nazaa nae akaniacha watoto wawili akalanda mjini tuu
10. Nilinunua viwanja vyote vimepotea kila mali niliyo nayo hata kijiko sina nimerudi nyumbani kama mtoto kumbe nina above 30s....

Katikati hapo fursa za kwenda nje, uongozi kisiasa na kidini ni nyingi mnoo lakini hazikuwahi kufanikiwa... niliishi kwa mateso makali ya moyo... niligombana na kumchukia Mungu kiasi sitaki kusikia mtu yeyote akimtaja mbele yangu.

Nina mwanangu na rafiki angu mwaka wa saba sasa hana mtoto na hata hawazi, akiwa hana hela hawazi akizipata anajipongeza ka kesho atapata tena akanigundisha kwamba je nikijipa stress hua nabidilisha jambo linalonisumbua?? Kama sina hela napata?? Au naishia kuumia tuu?? Jibu lilikua NO haibadilishi kitu.

Nikawaza kwamba wanaopitia magumu Mungu kwao haoni??

From that day, amani na utulivu wa nafsi ni kitu muhimu na namba moja, mbili naishi nikiwa sitegemei jambo lolote kuubwa maishani mwangu ila najikuta tuu matatizo yanaji set yenyewe.
 
Huu uandishi wako,hauleti maana ya unachokiandika!na unamuaibisha huyo Yesu mwenyewe.
Huyu Jamaa kwa uandishi wake nimemjibu kwa lugha anayoielewa! Naona kinyaa na kichefuchefu watu wanavyoteswa na shetani wakati Yesu anawaita wanamkataa alafu wanakuja JAMIIFORUMS kutafuta msaada! Si wamemchagua shetani? Acha awashughulikie na wanyamaze kimya na kuzimu wataenda wakiwa wanajitambua! Joannah
 
Kaokoke wewe Fala! Mnaambiwa mkimbilie Yesu mnakataa! Unadhani huko uendako ndo kuna unafuu? Utaishia kuzimu motoni! Tafuta kanisa la walokole wakuombee na uokoke! Fala wewe! Eti mnamkataa Yesu! Ona sasa!
shukrani kiongozi 🙏 nitajitahidi 🙏
 
namba 1,2,3,4,5 tuna fanana mimi niliungua na uji nikiwa na miezi 9 hadi leo nina kovu bega la kushoto na kichwani...!

aisee wewe ni pacha wangu... elimu zangu zote nimesoma kwa kuunga unga. kwakweli wewe na mimi tuna vitu tunashare... kabisa...!​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…