Nahitaji connection ya kumuhamisha wamoyo wangu, yupo huko machakani, nimechoka upweke, dau lipo

Wakuu wa kazi, upweke utaniua mwenzenu na nimeokoka sitaki kuwa na nyumba ndogo

Mwenzangu ni mwalimu huko machakani, elewa neno machakani, ni machakani haswaaa.

Sasa nilijipa matumaini atafanikiwa kuhama baada ya tangazo fulani la msawazo mwaka jana, ila tangu ajaze lile tangazo huu ni mwezi wa sita unaenda ukiisha bila uelekeo wowote, ni kama vile tumepigwa chenga ya mwili.

Niliamini kwamba angetendewa haki ya kufikiriwa uhamisho kwani alikuwa na vigezo vyote sitahiki lakini naona ni kama hili suala halitafanikiwa.

Hivo natangaza kama kuna anayeweza kunipatia connection ya kufanikisha jambo hili. Naomba kupata mtu serious wa kunifanikishia hili suala likakamilika, maana nimechoka na hizi sarakasi za yeye kwenda halmashauri kila siku.

Dau lipo kama unaweza kusaidia njoo DM
Umeokoka hutaki nyumba ndogo, ila kutoa rushwa unataka.

1+1=3-1, dhambi ni dhambi mura
 
Wakuu wa kazi, upweke utaniua mwenzenu na nimeokoka sitaki kuwa na nyumba ndogo

Mwenzangu ni mwalimu huko machakani, elewa neno machakani, ni machakani haswaaa.

Sasa nilijipa matumaini atafanikiwa kuhama baada ya tangazo fulani la msawazo mwaka jana, ila tangu ajaze lile tangazo huu ni mwezi wa sita unaenda ukiisha bila uelekeo wowote, ni kama vile tumepigwa chenga ya mwili.

Niliamini kwamba angetendewa haki ya kufikiriwa uhamisho kwani alikuwa na vigezo vyote sitahiki lakini naona ni kama hili suala halitafanikiwa.

Hivo natangaza kama kuna anayeweza kunipatia connection ya kufanikisha jambo hili. Naomba kupata mtu serious wa kunifanikishia hili suala likakamilika, maana nimechoka na hizi sarakasi za yeye kwenda halmashauri kila siku.

Dau lipo kama unaweza kusaidia njoo DM
Machakani ndiyo wapi, mlokole gani una lugha chafu hivyo?
 
Rushwa ni dhambi ndugu yangu, umeokoka ila unahalalisha rushwa! Utaendaje mbinguni?
Naangalia maslahi mapana, je ni vibaya kujitoa kwaajili ya haki za wanao?

Na je Yesu hakusema, waacheni watoto wadogo waje kwangu???
 
Kabla ya kuwa na watoto sikuwahi kujua uchungu wa kuona mwanao akiteseka kwa kuishi mbali, ndo naelewa sasa. Ni nateso aise
Nakuelewa sana ndugu nilipitia hiyo changamoto ya kuishi mbali na familia kidogo nipate uchizi. Nashukuru kwa sasa nipo na familia.
Ni raha sana kulea watoto
Mungu akufanyie wepesi
 
Back
Top Bottom