Sidhani kama kuna kitu cha kutia mara moja kwenye kisima ili kuondoa chumvi, kwa sababu maji ya chini ya ardhi kuwa na chumvi huo ni mchakato wa asili, hivyo maji ya kisima huwa na chumvi kutokana na jografia ya eneo husika(aina miamba/kuwa karibu na mwambao wa bahari/sababu nyingine..)
Mchakato wa kuondosha chumvi kwenye maji, ni kwa maji yenyewe baada ya kutoka kisimani, ila sio kwa kisima na maji yaliyomo maana huko ni kupingana na jografia, kitu ambacho ni muhali.
Hivyo zipo njia za kutumia vifaa maalumu ili kuyachuja maji kuondosha chumvi.