Nahitaji diet simple kwa sie wenye kupunguza vitambi


Asante mkuu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] conclusion ya kizembe. Nimejikuta tu naukumbuka huu uzi wangu
 
anza na kutokula mlo mzito usiku kama wali ugali machapati n.k badala yake kula vitu vya asili au matunda na kwa kiasi kidogo tu sio unakula mpaka ukilala chali unahisi kama kuna mtu kalala juu kumbe mivyakula imekaa kifuani...

ukishapunguza kula usiku vyakula vizito..
dili na maji ya vugu vugu kila asubuhi kunywa nusu lita kwa kuanzia na mchana kula chakula chochote lakini usile kama mwanzo..yani kama mwanzo ulikuwa unakula tonge mia sasa hivi fanya tonge sabini tu hapo utapungua taratibu....ukijifanya kutaka kupungua haraka utashindwa ..lazima uanze taratibu ili iwe tabia yako....

siri ya wenye vitambi ni kula sana tu ..
 
Mkuu asante ila siku zote huo ndio utaratibu wangu. Huwa sili jioni vyakula hivyo
 
Kupungua mwili sio tatizo kbs.....kudumu katika lifestyle ambayo mwili unapungua au unabaki constant ndo ishu....unaweza kuanza mazoezi lakini jiulize,je utafanya mazoezi maisha yako yote?watu wengi hawajui kwamba ukitaka upungue mwili cha kwanza na muhimu ni diet..hakikisha una style yako ya kula ambayo itapunguza mwili au kuuacha ulipo kwa zaid ya miaka na miaka....mazoezi kwa nyie wanawake wa kibongo kwenu ni km mateso tu..maji,mboga za majani,protini +wanga mdg +kuachana na tv+kazi ndogo ndogo umefua,umepika,umeenda sokoni kwa miguu,ukitoka kazini badala ya kupandia kituo cha karibu unatembea hadi kinachofuata,umerud umedeki nyumba nzima..be productive sio tu utapungua lakini utakuwa na mood mzuri.....sio chips kuku+jf mda wote+tamthilia+beki tatu
 
Asante mkuu nimekusoma
 
Tena ukiweza kutembea tembea, na msipende kudeke kwa kusimama, piga deki na dekio (tambara) ni mazoez mazuri sana,
Mimi huwa naacha mop pemben nainamisha mgongo wangu nadekii kote labda kama uvunguni sifikii nitapeleka mop hizi za wenzetu.

Mazoez madogo madogo yanasaidia pia
 
Ni lifestyle tu ndo unatakiwa kubadili mfano asubuhi kufanya zoezi hata 15mins mda unaamka, chai usiweke sukari kunywa na vitafunio ila sio ving sanaa kiasi tu hakikisha unashiba ,mchana kula matunda ya kutosha mpaka ushibe usile chakula thn usiku ukisikia njaa sana unaweza kula kidogo au kama huna njaa kunywa maziwa mgando ......

Trust m u must get that body every girl wish to ........
 
Mkuu maisha yangu yooote sijawahi kuishi na msaidizi wa kazi za ndani...si nyumbani kwa wazazi, nilikokulia wala kwangu kwa hiyo kama kazi za nyumbani ni zoezi ningekuwa kamodo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…