Nahitaji gari la kutembelea la juu kwa Bajeti ya Shilingi Milioni 30

Nahitaji gari la kutembelea la juu kwa Bajeti ya Shilingi Milioni 30

Wadau ninahitaji gari ya kutembelea ya juu nina tuhela nimepata baada ya kuuza kiazi, naomba ushauri maana mimi ni mweupe sana kwenye ujuaji wa magari ila napenda vitu vizuri licha ya kuwa mimi ni mkulima
Ungekua ni mtu wa magari ningekwambia uchukua BMW X3 Mnyama hatari sana, ila kama sio mzoefu wa magari chukua harrier 2.5.
 
Ungekua ni mtu wa magari ningekwambia uchukua BMW X3 Mnyama hatari sana, ila kama sio mzoefu wa magari chukua harrier 2.5.
Mkuu unaweza kudadavua kidogo unamaanisha nini unaposema kama 'mtu wa magari' achukue BMW X3, na sio achukue Harrier?
 
MISSING IMPOSSIBLE... unanikumbusha ENZI ya Kutafuta RUPIAH.. na PESA ZA ZAMANI...Ukiipata VISINGIZIO HAVIISHI,, .pengine hapo ULIPO HATA MCHANA HUJALA,,,unataka KUSUMBUWA WENZIO,,, KAMA una 30 MILLIONS kuna haja ya kutaka gari ya mkononi?
 
Mkuu kwani kuna sehemu nimeandika nataka gari ya mkononi au unajichetua tu kama ......jiongeze acha tabia za kike
 
Kama ni kweli unataka gari ya juu ya 30M chukua Discovery 3 ya 2.7 Diesel engine, iko vizuri sana kuanzia Ulaji wa mafuta, heshima mtaani mpaka uwezo wa kuhandle barabara mbovu e.t.c
 
Kama ni kweli unataka gari ya juu ya 30M chukua Discovery 3 ya 2.7 Diesel engine, iko vizuri sana kuanzia Ulaji wa mafuta, heshima mtaani mpaka uwezo wa kuhandle barabara mbovu e.t.c
Hapa hakikisha iwe Diesel, ikiwa Petrol utafurahia na roho yako
 
Mkuu unaweza kudadavua kidogo unamaanisha nini unaposema kama 'mtu wa magari' achukue BMW X3, na sio achukue Harrier?
X3 inahitaji mtu ambaye kutoa Milioni 2 kwa ajiri ya repair hashangai, pia ni gari zinazohitaji uelewa wa magari ili uwezo kuenjoy, mfano ukienda kwa fundi kama sio mtu wa magari atakupa ushauri wa kitoyota toyota wakati wewe umeenda na BMW X3, Kuna gari nyingi za Europe zimebadilishwa mifumo yake kwa sababu ya mafundi uchwara wengi.
 
Nunua Mark X , Crown au Brevis ndio Habari ya mjini na chenchi inaludi. Sema wenye Passo watakwambia gari yako inakula sana mafuta......wewe wajibu tu, “mlitaka ile nini mkate?”
 
Shukrani Mkuu ila nyuzi ni nyingi mnoo si rahisi kuzipitia zote hususani sisi wakulima
Acha uvivu.
Sasa unataka watu warudie mada mara tatu tatu kwa ajili yako kwani unawalipa?
Kwa nini unataka watu wakutumikie bila juhudi yoyote toka kwako?
Usipofanya juhudi ya kujua ni aina gani ya gari unahitaji, kwa matumizi yapi, kwa barabara zipi na hali ipi ya hewa..hiyo gari itageuka janga.
 
Back
Top Bottom