Nahitaji gari la kutembelea la juu kwa Bajeti ya Shilingi Milioni 30

Nahitaji gari la kutembelea la juu kwa Bajeti ya Shilingi Milioni 30

Acha uvivu.
Sasa unataka watu warudie mada mara tatu tatu kwa ajili yako kwani unawalipa?
Kwa nini unataka watu wakutumikie bila juhudi yoyote toka kwako?
Usipofanya juhudi ya kujua ni aina gani ya gari unahitaji, kwa matumizi yapi, kwa barabara zipi na hali ipi ya hewa..hiyo gari itageuka janga.
Mkuu mbona unatoa povu kwani ni lazima uandike? acha roho mbaya mkuu.
 
Nunua Mark X , Crown au Brevis ndio Habari ya mjini na chenchi inaludi. Sema wenye Passo watakwambia gari yako inakula sana mafuta......wewe wajibu tu, “mlitaka ile nini mkate?”
wadau wanasema hizi ni gari za vijana mimi umri umeenda sana
 
Mkuu mbona unatoa povu kwani ni lazima uandike? acha roho mbaya mkuu.
Kama sio lazima mimi kuandika basi usingetuuliza swali, na vile vile sio lazima na wewe kutuuliza maswali yako.
Sijatoa povu, ninakupa ushauri muhimu sana.
Tatizo lako hutaki kufanya kazi, kujishughulisha.
Hata google tu hutaki kutumia, wameshakushauri thread zimo humu hutaki kusoma unasumbua watu tu.
Hata aina ya gari na matumizi yake hujui. Sasa we unataka ufanyiwe kila kitu.
 
Mkuu sisi wakulima huwa hatuna muda kabisa tunapenda kuwatumia wataalam waliotakamika kama ninyi mtushauri ipasavyo hivyo usichoke kutumika
 
Wadau ninahitaji gari ya kutembelea ya juu nina tuhela nimepata baada ya kuuza kiazi, naomba ushauri maana mimi ni mweupe sana kwenye ujuaji wa magari ila napenda vitu vizuri licha ya kuwa mimi ni mkulima
Kanunue trekta uboreshe kilimo chako.
 
Kama ni kweli unataka gari ya juu ya 30M chukua Discovery 3 ya 2.7 Diesel engine, iko vizuri sana kuanzia Ulaji wa mafuta, heshima mtaani mpaka uwezo wa kuhandle barabara mbovu e.t.c

Mkuu GT, wapi zinapatikana? South Africa, Online-Japan au yard bongo?
 
Aisee mil30 ni tuhela[emoji124][emoji124][emoji124]
Ukinunua gari naomba niwe driver wako
 
Back
Top Bottom