Nahitaji kuanzisha biashara ya dagaa waliokaangwa kutoka Bukoba - Dar, natafuta soko na partnership wa kuuza hii bidhaa yangu

Nahitaji kuanzisha biashara ya dagaa waliokaangwa kutoka Bukoba - Dar, natafuta soko na partnership wa kuuza hii bidhaa yangu

shafii77

Member
Joined
Mar 18, 2019
Posts
60
Reaction score
85
Habari ndugu, kama kichwa Cha tangazo kilivyoandikwa nahitaji kuanzisha biashara ya kuuza dagaa waliokaangwa kutoka Bukoba -Dar hivyo nahitaji watu wa kushirikiana nao kupata soko, dagaa ni rejareja kwenye packet au kwa jumla pia wanapatikana kuanzia ndoo ya lita 10 mpk 20, hivyo kwa ambae yupo tayari especially women, but not necessarily naomba tusaidiane kusongesha maisha kupitia dagaa, NB, mtaji Kila kitu kipo ishu soko tu kwa mawasiliano nichek, 0674115095. Karibuni kwa maoni pia bandugu.
 
Habari ya leo wanajamii forum ?natumaini tunaendelea kupambana na kuendesha gurudumu liende mbele.
Waswahili wanasema ili usianguke na baiskeli hauna budi kukanyaga pedeli ili isonge mbele na ukiacha kukanyaga lazima udondoke.Hivyo endelea kukanyaga MUNGU WA WOTE Haijalishi kiasi gani tunamkosea lakini anasamehe na kututendea mema pale tunapo jishughurisha.

EMBU TUANGALIE VITU VYA KUZINGATIA KWENYE BIASHARA YA DAGAA KUPELEKA MKOANI KUTOKA MWANZA ZIWA VICTORIA.

1.
LESENI NDOGO YA KUSAFIRISHA DAGAA NDANI YA INCHI .Hii ni leseni ambayo upatikanaji wake ni rahisi kwa sababu ofsi zao zipo hapa KIRUMBA MWALONI MWANZA kwenye soko kuu la kimataifa la samaki na dagaa.Ambapo gharama yake kwa sasa ni shilingi elfu thelathini (Tsh 30,000/=).
Ukiwa na hiyo leseni unapeleka kila mkoa ndani ya Tanzania.

2. Kibali cha kusafirishia mzigo wako .hii document ni rahisi kuipata pia ndani ya dakika chache pia maana ofsi husika zipo hapa MWALONI KIRUMBA MWANZA Kwenye soko kuu la samaki na dagaa la kimataifa.(gharama ni ndogo pia ila inatozwa kulingana na mzigo wako ulivyo ukubwa).

3. Lipia ushuru wa mzigo wako unao usafirisha.kulipia ni rahisi pia maana wahusika wapo hapa hapa.

UKIWA NA HIVYO VITU KUFANYA BIASHARA YAKO NI RAHISI NA HAYUPO WA KUKUSUMBUA.

KWA WALE WANAO HITAJI DAGAA TAFADHALI NIPIGIE 0657886964.

SMS SITOJIBU HIVYO PIGA SIMU HIYO.
 
Back
Top Bottom