Mkuu [mention]EvilSpirit [/mention]wasikutishe kuwa ni siri, mambo yapo wazi. Tuanze na vyeo kisha majukumu:
Awali: How to address a TPDF soldier, formula ni NAMBA YA AJIRA kisha CHEO kisha MAJINA YAKE. Mfano “MT 89765 SGT KUFIR RAH”
* Askari wa JWTZ asiye na “V” hata moja anaitwa PRIVATE (PRAIVETI) - PTE.
* Mwenye V moja (cheo hiki kilikuwepo zamani, siku hizi kimefutwa) aliitwa LANCE CORPORAL (KOPLO USU) - L/CPL.
* Mwenye V mbili (anayefuata baada ya PTE kwa mfumo wa sasa) anaitwa CORPORAL (KOPLO) - CPL.
* Mwenye V tatu anaitwa SERGEANT (SAJINI) - SGT.
* Mwenye V tatu pamoja na alama ya bibi na bwana kwa juu anaitwa STAFF SERGEANT (SAJINTAJI) - SSGT.
* Anafuata mwenye kolokolo (kitu kama saa huvaliwa mkononi). Cheo hiki inaitwa SERGEANT MAJOR / SARMAJOR (SAMEJA). Hawa wamegawanyika sehemu mbili:
* A. Warrant Officer I (Daraja la Kwanza) - kolokolo lake lina alama ya mwenge (kwa mbali kama wa BoT)
* B. Warrant Officer II (Daraja la Pili) / kolokolo lake lina bibi na bwana.
Cheo cha Warrant Officer ndio mpaka kati ya vyeo vya Maafisa wa Jeshi (Army Officers) na Askari Wapiganaji (Vyeo vya Chini).
Muendelezo huu unaanzia vyeo vya Maafisa wa Jeshi:
* Nyota moja anaitwa LUTENI USU (2nd LIEUTENANT)
* Nyota mbili anaitwa LUTENI (LIEUTENANT)
* Nyota tatu anaitwa KAPTENI (Captain)
* Bibi na bwana (begani) anaitwa MAJOR (MEJA) - huyu ni kiungo katika medani za mapigano jeshini.
* Bibi na bwana + nyota moja anaitwa LUTENI KANALI (LT. COLONEL).
* Bibi na bwana + nyota mbili anakuwa KANALI (COLONEL).
* Bibi na bwana + nyota moja + mkasi anaitwa BRIGEDIA (JENERALI)
* Mkasi na bibi na bwana + nyota mbili anaitwa MAJOR GENERAL
* Ikiongezeka nyota moja hapo (jumla tatu) anaitwa LUTENI JENERALI
* Ikiongezeka nyota moja kwa juu (mkasi + bibi na bwana + nyota nne) anaitwa JENERALI, ambaye huwa ni mmoja tu MKUU WA MAJESHI YA ULINZI (CDF).
Jisomee zaidi hapa:
Rank and insignia of the Tanzanian Armed Forces | Wikiwand
UZI UJAO NITATOA KAZI ZAO.
View attachment 1905101
....
View attachment 1905102