Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

Khabari zenu,

Nimekuwa mtu wa kujisikia vibaya sana nikiuangalia mwili wangu. Mimi ni kijana wa miaka 28, nina kilo 93.

Nimenenepa sana. Nina kilo nisizozipenda, nimetumia mbinu ya mazoezi Ila nahisi kushindwa cuz ratiba za kujitafutia ridhiki zinabana. Natamani Nipungue nifikie hata kilo 75.

Mwili unanifanya nikivaa sipendezi kabisaa. Shepu mbaya, nina umbo la Kiazi sieleweki. Kitambi kikubwa.

Kuna jamaa yangu aliwahi nambia ili nipungue kwa haraka niwe nakunywa konyagi na nivute bangi ila nimefanya hivyo hakuna matokeo yoyote zaidi ya kujiumiza kuwa mlevi tu (Nimeacha).

Mwili nadhani unafanya mpaka nikiwa na mpenzi wangu kitandani simfikishi maana dakika 2 tu nishakojoa. Naumia na hii hali. Naombeni mbinu jamani, najua kuna watu humu walikuwa kama mie au zaidi ya mie.

Kitambi ninacho, nina maziwa makubwamakubwa yaani aibu siipendii hii hali naumia sana.

Miaka kadhaaa nyuma nilikuwa kawaida tu. Sikuwa kama sasa ila nashangaa nazidi kufumuka mwili yaani mpaka nakuwa na kibamia.

Uzi na picha.

View attachment 2646189
Kwa mujibu wa picha yako ni kama ulikuwa bonge sana mwili ukashuka

Kuindoa hiyo ndambi na kifua
Unahitaji mazoez sana ngozi ijivute

Hapo sasa inabid lishe pia izingatiwe sana
 
Mimi nadhani maeneo unatakiwa kufocus ni mawili hapo, kwanza Gym, kubali kuingia gharama ya gym ya kisasa ambayo watakupa trainings za kukata huo mwili na kukupa athletic body maana una mwili mzuri tu wa kukatika na kutengeneza mbavu.

Pili tazama sana ulaji wako ufanye kucut down Calories intake na fats.
 
Anza kwa kuangalia menu yako kisha mazoezi

Japo kuna wale unene upo tu kwenye koo na family zao
Kama na wewe kwenye uzazi wenu mpo hivyo wanene option iliyopo ni kujikubali
Mambo?!
 
Utamfanya apate vidonda vya tumbo sasa,,,,Acha kabisa vitu vyenye sukari,chocolate,soda,bia n.k,,,,Kula mchana ila wanga iwe kidogo tu mboga mboga na matunda kwa wingi,na jitahidi kabla ya kula unywe maji yatafanya ule chakula kidogo,pia ukiamka unywe maji ukipata ya uvugu vugu itakua vizuri,usiku usiguse chakula chenye wanga kabisa,,fanya hivo kama mwezi halafu kapime tena lazima upungue! Unaweza ukala hata mara5 na ukapungua inategemea na aina gani ya chakula unazokula N:B Ukinywa chai weka asali achana na sukari

Kuhusu mazoezi sio lazima uende gym,unaweza ukafanya nyumbani kwako kama dakika 30 unaruka kamba,push-ups kidogo n.k au ukatembea jion dakika 30 tu zinatosha.
 
I agrree...milo mitatu ni kwa saidia fundi na high performance athletes lakini sie wakukaa tunachapa marimba ya mzungu hapa jf au ofisini mlo mmoja tuu unatosha
Yap na hata saidia fundi anaweza kula milo miwili.

Kitu pcha msingi kwa watu wanaofanya kazi ngumu ni maji mengi,wengi hawanywi maji kisha wakiumwa na vichwa wanasema njaa,anapoteza maji mengi so ishu ya msingi ni maji mengi na chakula kiasi
 
20% ya weight loss ni mazoezi, 80% ni discipline kwenye ulaji ndo maana wapo watu wana attend Gym daily lkn hakuna matokeo chanya sawa na mategemeo yao, hii ni kwa sababu wamekosa nidhamu ya kudhibiti namna ya ulaji.

Kwa kuwa muda wako wa utafutaji unakubana kufanya mazoezi komaa na 80% ya nidhamu ya ulaji kama ifuatavyo;

Tumia njia ya ulaji ya pyramid kwamba kadri unavyokaribia masaa ya kulala ndivyo upunguze wingi Volume ya chakula. Hata hivyo volume hiyo isiwe ile uliyozoea kawaida kwamba lzm sahani iwe mlima. Best practice ni usk kula matunda pekee ndani ya mwezi utakuwa umekata hata 5kg

Sambamba na hilo Punguza kbs matumizi ya vyakula vya wanga, sukari vyakula vya kukaanga incl. Junk food, kula kwa wakati maana kuchelewa kula kunasababisha kula kilichopo na si unachokihitaji, Punguza au acha kbs kwa muda pombe hasa beer, soda na juice zote zenye sukari hasa zioe za viwandani lengo likiwa kujitathimini!

Ukipata walau 30min kimbia/tembea umbali hata wa km 3 kwa kuanzia awali itakuwa shida but as u go on itakuwa ni tabia na utanza ku enjoy that kind of lifestyle!

Haya ninayokwambia nimeyaishi na nimefanikiwa sana kwa ss nacontrol BMI iko vzr sana 22.3 which is btw the range!

NB
Asikudanganye mtu kuna dawa ya kupunguza uzito.. ni uongo only nidhamu ya kula na nidhamu ya mazoezi pia!
Nimekuelewa mkuu...
 
Lakini pia unaweza kuwatafuta forever living wana program inaitwa C9 itakufaa sana.. Japo bei imechangamka
Yeah nai0naga sana ila bei kubwa sana na kipat0 changu si rafiki kiiv0..
 
Vyakula vyako na vinywaji vyako ndiyo wabaya wako nambari moja. Ukiweza kutawala ulaji wako tatito lako limekwisha. Jiangalie ulaji wako na unywaji wako. Kuna vitu kama wali, chips, nyama, soda/juice, enegy, bia, nk.. Kama unatumia sana anzia hapo kurekebisha.
NB; HUWA NAAMINI NI UPUMBAVU KUFANYA MAZOEZI ILI UPUNGUE MWILI WAKATI UNAENDELEA KUONGEZA KULA/KUNYWA.
Fact...
 
Inamaana simu yako haina kitufe cha O mpaka uandike 0 sidhan kama kuna kupungua kwa uandishi huu
Wewe ni mla chips siyo bure
 
Kopa kausha damu utapungua faster 🤣

Jokes aside.. Huna unene wa kutisha bado, ni vyema umeanza kuchukua tahadahri sasa.

Punguza kula wanga na mafuta. Kula milo miwli, asubuhi chai kidogo, mchana piga fresh shiba kabisa, usiku usile kunywa chai au matunda kidogo sana. Hapa mwanzo lazima uwe mgumu.

Kama huna muda wa mazoezi jaribu kupiga push ups kila siku na pull ups kama mazingina yanaruhusu.
 
Back
Top Bottom