Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

punguza kula atleast mara 2 kwa siku au uwe na uwezo wa kuvumilia njaa ata cku nzima ili mwili utumie akiba ya chakula ulicho hifadhi mwilni,na ikiwezekana tafuta kazi ngumu uwe unafanya mfano kazi za kubeba zege hyo inaweza kukusaidia kupungua kwa urahisi.
 
Punguza kipimo cha chakula, uwe unakunywa na maji ya vugu vugu yenye limao
 
Mbona kuongezeka simple sana...
Weee kuongeza kilo nimtiti mkubwa kupungua ni ishu yakujipambania kwanguvu zako mwenyewe ila kuongezeka nimpaka mwili ukubal wenyewe ukute mtu anamastress au unaroho yakinyongo nakwambia hata ujilazimishe kuvimbiwa huongezeki
 
Khabari zenu,

Nimekuwa mtu wa kujisikia vibaya sana nikiuangalia mwili wangu. Mimi ni kijana wa miaka 28, nina kilo 93.

Nimenenepa sana. Nina kilo nisizozipenda, nimetumia mbinu ya mazoezi Ila nahisi kushindwa cuz ratiba za kujitafutia ridhiki zinabana. Natamani Nipungue nifikie hata kilo 75.

Mwili unanifanya nikivaa sipendezi kabisaa. Shepu mbaya, nina umbo la Kiazi sieleweki. Kitambi kikubwa.

Kuna jamaa yangu aliwahi nambia ili nipungue kwa haraka niwe nakunywa konyagi na nivute bangi ila nimefanya hivyo hakuna matokeo yoyote zaidi ya kujiumiza kuwa mlevi tu (Nimeacha).

Mwili nadhani unafanya mpaka nikiwa na mpenzi wangu kitandani simfikishi maana dakika 2 tu nishakojoa. Naumia na hii hali. Naombeni mbinu jamani, najua kuna watu humu walikuwa kama mie au zaidi ya mie.

Kitambi ninacho, nina maziwa makubwamakubwa yaani aibu siipendii hii hali naumia sana.

Miaka kadhaaa nyuma nilikuwa kawaida tu. Sikuwa kama sasa ila nashangaa nazidi kufumuka mwili yaani mpaka nakuwa na kibamia.

Uzi na picha.

View attachment 2646189
Mbona kwenye thread hii hapo chini ulisema ulikuwa unaenda gym na kukimbia?
 
Acha kula wanga aina zote (wali, ugali, chapati, maandazi, vitumbua, mihogo, viazi, chipsi, sambusa etc). In short vitu vyote vinavyotokana na ngano, sembe au grains
Acha kula sukari (usitumie sukari kwenye chai au maziwa.)
Acha kunywa pombe, soda, energy drinks, juice etc. Kunywa maji tu.
Usivute sigara
Ukifanya haya ndani ya wiki utakuwa na kilo 70.
Kinachounenepesha mwili ni wanga na sukari. It Mwili wa binadamu haukuumbwa kutumia wanga. Ndio maana ukila wanga insulin inazalishwa kwenda kuitoa sukari ile kwenye damu na kuibadilisha kuwa mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungemwambia ale nini sasa!asile wanga ale nini!!?
 
pata uji wa lishe wenye karanga mbegu za maboga mahindi ya njano ulezi mtama kidogo soya uweke prestige blue band ,maziwa fresh,asali pata na kipande cha mkate na yai la kukanga asubui saa nne pata kitu chochote kama mtori,punguza kidogo matembezi kwa mguu ..mchana kula kawaida weka na juice ya embe saakumi pata nusu lita ya chai ya maziwa saa moja na nusu pata msosi wako kawaida .miezi mitatu utanambia
Oya we jamaa ni Dr kweli 🤣🤣🤣
 
pata uji wa lishe wenye karanga mbegu za maboga mahindi ya njano ulezi mtama kidogo soya uweke prestige blue band ,maziwa fresh,asali pata na kipande cha mkate na yai la kukanga asubui saa nne pata kitu chochote kama mtori,punguza kidogo matembezi kwa mguu ..mchana kula kawaida weka na juice ya embe saakumi pata nusu lita ya chai ya maziwa saa moja na nusu pata msosi wako kawaida .miezi mitatu utanambia
waoh! Asante sàna boss kwa huu muongozo,nitafanya hivyo
 
Kakope hela usuyoweza kulipa usipopungua niite mbwa
 
Ishi kama unaumwa kisukari fata mashart ya mgonjwa wa sukari vizur sana

Baada ya wiki 3 njoo unipe majibu
Niko paleeeee
 
Yah,Niko kwenye ratiba ya uji wa lishe,kuna mdau pia alinishauri hilo
angalizo huo mchanganyiko ni mkali sana ni vyema ukawa unafanya na mazoezi ya kuruka kamba baada ya kutumia kwa mwezi ili kuepuka hatari ya kupata kitambi

pia meza dawa za minyoo aina zote kabla
 
Dah kumbe wengi tuna struggle eeeh..
Mimi mwenyewe dah napiga tizi sana Sasa hivi...
Bro ni msosi uwezo nenepa bila kula... control misos hiyo
 
Acha kula mchana,na usiku kula kiduuuuuuchu,asubuhi kunuwa maji ya asali na ndimu au limao,kama hujapungua Rudi Tena hapa

Utamfanya apate vidonda vya tumbo sasa,,,,Acha kabisa vitu vyenye sukari,chocolate,soda,bia n.k,,,,Kula mchana ila wanga iwe kidogo tu mboga mboga na matunda kwa wingi,na jitahidi kabla ya kula unywe maji yatafanya ule chakula kidogo,pia ukiamka unywe maji ukipata ya uvugu vugu itakua vizuri,usiku usiguse chakula chenye wanga kabisa,,fanya hivo kama mwezi halafu kapime tena lazima upungue! Unaweza ukala hata mara5 na ukapungua inategemea na aina gani ya chakula unazokula N:B Ukinywa chai weka asali achana na sukari
 
Hii mada inanihusu kabisa,nimepunguza msosi jioni naoiga matunda tu na whisky
 
Back
Top Bottom