Biashara ya kushauriwa wakati fulani siyo nzuri sana. Unatakiwa ukafanye utafiti mwenyewe ili uwe na uhakika wa kitu unachoenda kukifanya.
Ungetembelea hayo masoko ya Dar ili kujua bei ya kuuzia pamoja na usafiri, halafu ungeenda huko Lindi ili kuangalia upatikanaji wa hizo nazi. Baada ya hapo unafanya sasa tathmini kuona kama hiyo biashara itakulipa, au la.