Nahitaji msaada wa kisheria nahisi kunyanyaswa na mwanamke kwenye usafiri wa uma

Sasa mkuu ulitaka alivofosi kupita aende wapi na ulishasema kuwa basi lilikuwa limejaa? Ukiwa hutaki kupata usumbufu kwenye usafiri wa umma ni vyema kutumia usafiri wako binafsi ndio hutopata kash kash kama hizo.

Kuna siku jioni natokea magomeni kanisani naelekea kimara nimepanda mwendofyade imejaa sana nikawa nimesimama jirani na dada mmoja mbandika kope na kucha akawa ananisukuma sukuma tusigusane utadhani humo ndani tupo wawili tu hadi waliokuwa wamekaa wakawa wanashangaa, kama kawaida yangu ni mkimya na mvumilivu sana nikajisemea hapa siongei chochote hadi pale atakapologwa na kufungua mdomo wake.

Wakamloga bhana kamdomo, akaniambia kaka usiniguse guse sitaki kabisa mwishowe tuje tubanduane kucha hapa, nikaona huyu namlea nikamwambia dada ungetaka kuepuka kuguswa guswa ungerequest bolt au ungetumia usafiri wako akajibu uo usafiri ulininunulia wewe? Nikamjibu hilo sipaswi kulijua mwendokasi haina VIP kwahiyo tulia kwa tulivyojazana vumilia ukishindwa shuka.

NB: unapochukua uamuzi wa kutumia usafiri wa umma kama daladala na mwendokasi hasa kwa huko dasalama ni vyema kabisa kuvumilia uhalisia wa usumbufu wa usafiri huo, kubanana ni kawaida, kukanyagwa, kusukumwa, kunukiana jasho na mengineyo. Ukija na uzungu wako lazima upate shida zaidi maana kutumia tu aina hiyo ya usafiri tayari ni shida.
 
🤣 kenge kabisa ati dungadunga!
 
Dah Leo nusu albino a.k.a kubwa la manusu, ume tema nondo aisee😆
 
Huo ni ukatili kabisa fuatilia na usiache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…