Kwanza tambua hakuna mtu anajali kuhusu wewe, sasa wewe kwanini uwajali wao kuhusu wewe. Ukifika umri fulani utathibitisha hili.
Wekeza muda wako kikamilifu kufanya vitu unavyovipenda.
Epuka kampani ya watu wasiojali thamani yako, ni bora ukawa karibu na mbwa kuliko watu kama hao.
Usipende kuhesabu madhaifu yako badala yake anza kuhesabu baraka ulizo nazo haijalishi ukubwa wake.
Usijilinganishe na mtu, kila mmoja ni unique kwa namna yake.
Jiongeze thamani kwa kuongeza maarifa na ujuzi.
Usioneshe kutegemea mtu, jione kwamba wewe ndio unategemewa.
Chochote utachofanya, fanya kama mfalme lakini asiye na majivuno bali mnyenyekevu.
Point kubwa iliyobeba zote: Ishi sasa, usiishi kwa kuangalia mapungufu yako ya jana wala usiwe na hofu na kesho. Ukiweza hapa basi umemaliza kila kitu.