Nahitaji msaada wa kuongeza confidence na kujiamini

Nahitaji msaada wa kuongeza confidence na kujiamini

Kama unaanza kutafakari kitu unachokiongea kwamba watu wanakuchuliajeee unapoongea na unaogopa kukosea hutaweza

Kinachotakiwa ni kujilipua tu na kutoangalia macho ya watu kwa kuangalia juu ya macho yao
Ni Kweli kabisa. Kwanza unatakiwa ujue hadhira yako ni aina gani ya watu/level ya ufahamu wao. Hotuba iandane na mifano ya maisha yao halisi. Ushauri wako wa kujilipua tuu siungi mkono unaweza kujipiga risasi sokoni ukatoa boko
 
vp bingwa! we LUMBANA, LUMBANA, LUMBANA, LUMBANA...>>
nakwambia ivii! we lumbana nao tu. jitahidi KUJUMUIKA na jamii yako, anzisha hoja ya msingi kisha jadili nao.utapata kujiamini.
 
Introvert akilewa anakuwa na makelele na fujo yaani full confidence.

Jiangalie kwenye kioo, smile then Ongea harafu jijibu mwenyewe.

Ukiongea na mtu usimuangalie kwenye macho yake bali angalia kwenye paji la uso au nywele zake.

Anza na hizo, you can do this.
 
Ni Kweli kabisa. Kwanza unatakiwa ujue hadhira yako ni aina gani ya watu/level ya ufahamu wao. Hotuba iandane na mifano ya maisha yao halisi. Ushauri wako wa kujilipua tuu siungi mkono unaweza kujipiga risasi sokoni ukatoa boko
Watu wengi huwa wanadhani ninajiamini sana lakini huwa hawajui ndani yangu huwa najionaje yaani mm confidence huwa inakuja ninapothubutu(kujilipua) bila kufikiri sanaaaaa
 
Mbona siku izi jamii ina watu wa hovyo sana mtu ameomba ushauri mnamkashifu naamini hili jukwaa kuna wasomi wengi wanaoweza kuchangia kutatua matatizo ya watu .sio kumvunja mtu moyo .humu kuna watu wazuri pia watu wasiojielewa naomba kama Huna msaandaa Acha kupost utumbo.tatizo lake si ajabu wapo watanzania wengi wanaitaji msaada kama yeye tujaribu kuchangia kutatua matatizo sio akili ya kukatisha watu tamaa
 
Habari zenu Wana jukwaa kama kichwa Cha Uzi kinavyosema naomba mnisaidie tips pamoja na vitabu nitakavyokua nasoma kuongeza confidence yangu pamoja na kujiamini
Natanguliza shukrani na nipo hapa kusoma Kila comment na ushauri mtakaonipa
Nilikuwa mwogamwoga kama wewe. Nilichokifanya;
1) nilianza kutongoza mademu randomly (si kwa nia ya kuwala, bali kunijengea confidence ya Kushawishi). Nilikuwa naenda mbali na makazi yangu ili hata nikikataliwa isijekuwa aibu mtaani.
2) kujiweka kimbelembele ili nifanye presentation endapo kama panahitajika mtu wa kupresent.
3) kuhudhuria kijiwe cha kahawa na kuchangia mijadala.
4) kwenda bar kukutana na watu tofauti tofauti. Kwenda bar siyo lazima unywe pombe, kuna maji, soda na juice pia.
Haya yaliboost sana.
 
Back
Top Bottom