SIFA ZA MWANAUME WA KUZAA NAE:
1. Awe na Akili Timamu
2. Awe tayari kupima Magonjwa yote ya Zinaa na mbegu zake kama nzima (tutaenda hospital pamoja)
3. Asiwe busy sana sababu nataka awe focused na kunipa ujauzito zile siku zote za upevushaji tutakazokutana
4. Asinipende na kutaka kunifanya girlfriend wake mara aje na sera za kutaka ndoa sijui kunibadilisha
5. Asiniombe Pesa kwenye jambo hili, kwani mimi nitakua nina safari ndefu ya kulea Mtoto siwezi kununua mbegu
6. Azingatie Mimba ikiingia mimi na yeye tunakata mawasiliano
7. Umri usizidi miaka 40 sitaki Mtu mwenye changamoto zozote za kiafya
SIFA ZANGU:
1. Nina Akili Timamu
2. Lesbian
3. Ready kuwa Mama
4. Umri miaka 28
5. Nipo Dar es salaam
MREJESHO:
Shukrani wadau mtu nimempata ila katoka nje ya JF kuna mtu nafanya nae kazi, aliniconnect na ndugu yake, tulipatana tangu december ila tukasubiri vurugu za mwisho wa mwaka zipite ndio tuanze zoezi letu la vipimo na sio muda zoezi lenyewe litaanza [emoji2960]
Huyu Kaka ana Akili timamu, ni daktari wa kina mama katika hospital fulani, hajaoa wala hana mchumba, tumeenda dates mbali mbali kwanza ananukia vizuri, hana mandevu, hanuki mdomo, ni bonge la gentleman, ametulia ila sio mpole kwa hiyo hatukosi story kila tukichat na tukipigiana simu, kuna chemistry ndani yetu which is good kwa tunachotaka kukifanya....
Amenikubali vile nilivyo, hana swaga za "nataka kukubadilisha", ananiheshimu sana, hofu yangu asije aka fall in love tu maana ana speed [emoji1]
MNAO TEXT NA KUCALL ACHENI MARA MOJA, KAZI IMESHAISHA TUSUBIRI MAJIBU TU.