Habari za jioni ndugu zangu wana MMU.
Bila kupoteza muda ni kwamba nina miaka 30, mkiristo, nina elimu ya chuo, nimejiajiri mwenyewe, nina urefu wa wastani.
Hivyo basi, kutokana na hizo sifa hapo zilizotajwa hapo juu napenda kuwataarifu kwamba nahitaji rafiki wa kike ambaye siku za mbeleni atakuwa mke wangu kama tutakuwa na maridhiano.
Nitafurahi sana kama nitampata rafike mwenye sifa zifuatazo:- awe na umri wa miaka 24-29, awe mwanasheria/daktari/mwalimu/mhasibu, awe ni mcha mungu, asiwe mweupe sana wala mweusi sana, pia awe mrefu wa wastani.
Kadhalika, sipendi rafiki mwenye mtizamo hasi na usio sahihi (uongo, lawama, chuki, kununa bila sababu, unafiki,gubu na umbea) bali napenda rafiki ambaye atakuwa na mawazo chanya, mazuri na yenye kujenga na mwenye ustaarabu mwingi na staha.
Aidha, napenda rafiki ambaye ni muwazi sana nikimaanisha kwamba ambaye yupo tayari kueleza makosa yangu au kuniambia ukweli mtupu bila kupepesa macho pale ambapo nitakosea.
Mwisho, nina dhamira nzuri na nimedhamiria katika jambo hili kwa lugha nyepesi nipo tayari kujenga huo urafiki ambao utakuwa imara kuelekea katika maisha ya ndoa.
Karibuni sana PM.
Ahsanteni.