Naibu Nishati: Tumelazimika kutafuta wakandarasi wa bei kubwa lakini kwa uharaka. Aahidi kadhia ya umeme kukoma Januari

Naibu waziri wa Nishati amewaomba watanzania kuwavumilia na kwasasa wanarekebisha mitambo ya gesi yenye matatizo na wanaamini kufikia Januari tatizo kama litakuwa halijapungua kabisa litakuwa limekwisha.
Kheee 😳😳 c walisema December?
 
Hahahahahaha naona MAGAS TURBINE ambayo hayana hata 5yrs yameanza kusumbua sasa....hivi hata warrant yamemaliza kweli au tumeviolate warrant tayari kama lile Dilimulaina la long haul tukalipeleka short haul Mwanza tukaua engine.... Hahahahaha naona anatafutiwa mtu service contract ya kurun Kinyerezi huku Tanescrow wakibaki ofisini kusubiri kulipa invoices... hahahahaha

What kind of species we are gents...
 
Utopolo mtupu! Hao wakandarasi wa gharama kubwa watoka wapi kama sio kupiga Hela! Si mlisema vyanzo vya maji vimeharibiwa Kwa Kasi?

Je Ina maana hao wakandarasi wanaleta maji kujaza bwawani au?? Tuambieni na gharama yao halisi.!
Hii ndio Tanzania buana!!!
 
Sijui akili za hawa watu ziko wapi,au sisi wananchi ndo wametuzalau sana.maana sio kwasalakasi hizo zisizo na muunganiko wowote.
 
Soon watasema tatizo la umeme linatokana na vita ya Ukraine na Urusi
 
Na siku CCM ikitoka madarakani haitarudi tena mbwaaa hawa.
Na wenyewe wanajua hilo ndio maana wanang'ang'ania madaraka kwa hali na mali, wako radhi tuingie vitani kuliko kuachia nchi.

Maana wanajua wakitoka, labda ipite miaka 1000 baadae, baada ya vizazi kupotea na wananchi kusahau kila kitu ndio watarudishwa tena.
 
Wameshatupiga hapo.

Kama tatizo halijapungua basi litakuwa limekwisha.

Kauli inamaana tatizo ni endelevu.
 
Kipara ni bingwa wa uongo

Lakini ilikuwa wazi TANESCO (like any other technical industry) sio ya kuongozwa na mtu ambae aijui hiyo sector.

Ili uwe manager wa technical sector kuna mawili either umesomea degree ya industry husika (in this instance electricity engineering) ukafanya kazi na in the process shirika likakupekeka kwenye development skills za kusomea management skills and then you ascend to the top post with their succession planning (ndio utaratibu wa wizara zote).

Njia ya pili ya kushika hiyo nafasi ni kusomea management degree ya sector husika. Hizi ni degree za kibiashara lakini zina focus on industry supervision and thinking.

Ukisoma management ya nishati utajua basics zote za usimamizi, strategic planning, laws and regulations (both local and international) definition ya success na vitu vya kuchunguza ata kama sio mtaalamu ulisomea mambo ya umeme (in this instance).

Kwa sie ambao tushafyatua hizo degree za management upande wa afya, biashara, oil and gas, na nyingine nyingi za ovyo ovyo; tukiwasikia tu hao watu unaona amna kitu.

January has ideas na ni msikivu ukimkosoa kwa point anabadili mbinu. Hiyo ndio nature yake ukimuelewa hizo ni sifa za uongozi; ila shida yake ni urafiki.

Raisi Samia kaitafutia nchi hela nyingi sana angekuwa na dira, uwezo na mkali angefanya makubwa sana (kama asingebadili njia aliyoikuta), sema bahati yake ni ya mkono wa kulia na ya kutokea mkono wa Kushoto.

Ni hivi kwa sasa tuna watu wa ovyo mno wanaongoza nchi na sio makosa yote ni yao; ila ni mtazamo wao wa watu wanaodhani ni sahihi kwenye kuwasaidia na leadership style ya ‘laissez faire’ ndio shida zaidi

In other words watu wanao endesha serikali hawana uwezo.

Kitu nilichojifunza baada ya hizi chaguzi za CCM ni kwamba JK ni mshauri wa part time. Jakaya Kikwete asingeweza kumuacha mtu kama Nazir Karamagi ashike nafasi ndani ya chama tena (Karamagi alikuwa mtu wa ovyo sio mchezo) katika uraisi wake.

Tuseme inatosha kwa huyu ‘malkia wa nyuki’ hana uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…