Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Naibu wa rais Kenya amelazimika kukimbilia mahakamani kujaribu kuzuia mchakato wa kubanduliwa kwake ofisini ingawa uwezekano wa bunge kumuondoa bado ni mkubwa zaidi.
Tayari wabunge wapatao 242 wameridhia muswada huo kuletwa bungeni kati ya angalau wabunge 117 waliohitajika kisheria.
Endapo spika ataridhika kwamba matakwa ya kisheria yametimizwa ataidhinisha mjadala wa hoja na kupiga kura katika kikao cha mashauriano, na iwapo theluthi mbili ya wabunge yaani wabunge 233 kati ya 349 watapiga kura ya ndiyo ili Gachagua aondolewe mamlakani, basi ni mahakama pekee ndiyo inaweza kumnusuru asalie kwenye nafasi yake kwa mujibu wa katiba ya Kenya ya 2010.
Pamoja na mambo mengine, Naibu wa Rais huyo wa Kenya Rigathi Gachagua, anatuhumiwa kukiuka katiba, kukiuka sheria za nchi, utovu wa nidhamu uliokithiri, matumizi mabaya ya ofisi na tuhuma nyingine nyingine ambazo zitawekwa wazi na mtoa hoja mapema wiki ijayo.
Ni yapi maoni yako, ajiuzulu au apambane?🐒
Mungu Ibariki Tanzania