Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Naibu Waziri Mhe. Kigahe Awataka Wafanyabiashara Kutumia Fursa ya Soko Huru la Afrika
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe amewataka wafanyabishara, wajasiriamali na makampuni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki kuonyesha bidhaa zao,kujitangaza na kukuza soko la biashara kupitia soko huru la Afrika Mashariki.
Mhe. Kigahe amebainisha hayo Agosti 28, 2023 kwa niaba ya Waziri wa Biashara na Viwanda, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na chemba ya wafanyabishara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Aidha, Mhe. Kigahe amesema kuwa Maonesho hayo pia yanatoa fursa kwa kampuni za ndani kujifunza mbinu mbalimbali katika kukuza uuzaji wa bidhaa nje na kutumia fursa zilizopo za masoko ya Afrika Mashariki, SADC, AGOA na hivyo kila mwanachi hana budi kuchangamikia fursa hiyo ambayo inapanua wigo wa kufanyabiasha, kuwekeza katika nchi yoyote katika eneo la Afrika Mashariki, na fursa ya ajira kwa watu wa Afrika Mashariki Kwani Tanzania imeonekana kuwa na fursa nyingi za uwekezaji, kiusalama na mazingira bora kufanyabiashara.
Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza Ndg. Gabriel Kenene amesema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kutangaza biashara zao na kupata masoko mapya mbalimbali.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.31.jpeg30.7 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.32.jpeg42 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.32(1).jpeg40.5 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.33.jpeg40.8 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.33(1).jpeg56.3 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.34(1).jpeg37.2 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-03 at 13.25.35(1).jpeg48.9 KB · Views: 1