Rais Magufuli wakati yupo hai aliwaimarisha sana Wasukuma na kuwafanya wawe wamoja, sasa baada ya kufa walisambaa sana kama kondoo waliokosa mchungaji.
Sasa kule Kanda ya Ziwa Wasukuma bado wanaamini Magufuri hana mbadala, hawana habari kabisa na Rais Samia. Picha Hayati Magufuri bado zinatamba kwenye hoteli na saloon, wananchi wa kawaida bado hawapo na Rais Samia!
Sasa Rais Samia ametafakari vizuri kuwapelekea Biteko ili awakusanye awarejeshe kwenye ule umoja na kuwafanya waanze kuwa na imani nae na hii ndio kazi kuu ya Biteko, kuifanya Kanda ya Ziwa iwe mikononi na kuua kabisa Sukuma gang, maana kazi anayoifanya Waziri Mkuu Majaliwa ilikuwa haihtaji msaidizi.