Kujua kupika ni life skill.Hivi kupika Ugali kunahitaji mafunzo rasmi! Yule mama kijijini aliyelea Watoto alisoma VETA wapi
JokaKuu
Halafu kwenye uzi mwingine unakuja kutupanga wewe babu wa miaka 78+ 😹😹Kuna graduate mmoja wa chuo extremely gojazi and smart kwa jinsi nilivyokuwa namchukulia nilikuwa naamini kabisa kuwa hata kuchemsha mayai hajui maana kwao ni wa kishua kidogo na alikuwa dad's girl. Huwa akija kwangu tunaagiza chakula au tunatoka kwenda kula.
Sasa juzi kaja hapa naye akajifunga kibwebwe kanga moko kifuani na kusema nikamletee viungo eti anataka kupika pilau. Nilicheka sana (kimoyomoyo) na huyoo nikapewa list ya viungo vya pilau na makorokocho mengine. Narudi nakuta mchele keshaandaa; nikamsaidia kukata kata nyanya, vitunguu na baadhi ya viungo. Kisha nikaambiwa niondoke jikoni. Niliondoka huku nikicheka kimoyomoyo balaa maana nilijua tutakula maajabu.
Nilishangaa alipopakua. Aisee msomi yule anajua kupika pilau sijaona. Na kachumbari imetengenezwa ikatengenezeka. Na pilipili iliyopikwa. Nilishangaa sana; na mpaka leo sijaamini na tumepanga akija tena wikendi hii atapika laivu nami nikiwepo ili Utomaso uniishe. Tena anataka kunifundisha kupika tambi, nyama, dagaa na ndizi kwa kiwango cha juu.
Nilipomuuliza alijifunzia wapi kupika vile alisema kuwa pamoja na kwamba nyumbani kwao kulikuwa na wafanyakazi tena wawili lakini kila mtoto alikuwa na zamu ya kupika. Mama yao mpaka alikuwa analeta marafiki zake wanaojua kupika vizuri kumzidi baadhi ya vyakula wanawafundisha na akasema kuwa hata kaka zake wanajua kupika pia maana nao kuna wakati walikuwa na zamu japo mara moja moja.
Nilijifunza jambo kubwa sana katika malezi hasa haya ya kisasa ambapo watoto hawa ambao wazazi wao wana kauwezo wanelelewa kama vile wazazi wao wataendelea kuwepo milele na kuwa wanawapikia, kuwafulia na kuwasafishia.
Wazazi aisee badilikeni. Siku moja hamtakuwepo. Hawa mabroila wenu mnaowadekeza hivi wataishije?
Utafikaje Misungwi huku wakati upo Kariakoo Dar ukikusanya maokoto?Halafu kwenye uzi mwingine unakuja kutupanga wewe babu wa miaka 78+ 😹😹
Naomba invitation wifi akija tena nije kushuhudia utamu wa chakula atakachopika, nikimaliza kula mi nitakaa sebuleni nikiangalia movie wala sitowasumbua wakati akikutumbua upele chumbani..!! 😜😹
Hizi elimu zingine sio lazima ziwe formal. Wazazi wana mchango mkubwa katika suala hili. Wanaweza kumsaidia au kumharibu mtoto!Akiwa anazungumza leo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Miaka 50 ya Veta iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni kawaida kuona mtoto amemaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kujipikia chakula chake mwenyewe.
Amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) ina uwezo na jukumu la kubadilisha Tanzania kama jamii itakubaliana watoto kupata stadi fulani kwa ajili ya kuboresha maisha.
View attachment 3278812
Hivi huyu Neta anaongea nini?Kwahiyo waende VETA kupika?
Kuna graduate mmoja wa chuo extremely gojazi and smart kwa jinsi nilivyokuwa namchukulia nilikuwa naamini kabisa kuwa hata kuchemsha mayai hajui maana kwao ni wa kishua kidogo na alikuwa dad's girl. Huwa akija kwangu tunaagiza chakula au tunatoka kwenda kula.
Sasa juzi kaja hapa naye akajifunga kibwebwe kanga moko kifuani na kusema nikamletee viungo eti anataka kupika pilau. Nilicheka sana (kimoyomoyo) na huyoo nikapewa list ya viungo vya pilau na makorokocho mengine. Narudi nakuta mchele keshaandaa; nikamsaidia kukata kata nyanya, vitunguu na baadhi ya viungo. Kisha nikaambiwa niondoke jikoni. Niliondoka huku nikicheka kimoyomoyo balaa maana nilijua tutakula maajabu.
Nilishangaa alipopakua. Aisee msomi yule anajua kupika pilau sijaona. Na kachumbari imetengenezwa ikatengenezeka. Na pilipili iliyopikwa. Nilishangaa sana; na mpaka leo sijaamini na tumepanga akija tena wikendi hii atapika laivu nami nikiwepo ili Utomaso uniishe. Tena anataka kunifundisha kupika tambi, nyama, dagaa na ndizi kwa kiwango cha juu.
Nilipomuuliza alijifunzia wapi kupika vile alisema kuwa pamoja na kwamba nyumbani kwao kulikuwa na wafanyakazi tena wawili lakini kila mtoto alikuwa na zamu ya kupika. Mama yao mpaka alikuwa analeta marafiki zake wanaojua kupika vizuri kumzidi baadhi ya vyakula wanawafundisha na akasema kuwa hata kaka zake wanajua kupika pia maana nao kuna wakati walikuwa na zamu japo mara moja moja.
Nilijifunza jambo kubwa sana katika malezi hasa haya ya kisasa ambapo watoto hawa ambao wazazi wao wana kauwezo wanelelewa kama vile wazazi wao wataendelea kuwepo milele na kuwa wanawapikia, kuwafulia na kuwasafishia.
Wazazi aisee badilikeni. Siku moja hamtakuwepo. Hawa mabroila wenu mnaowadekeza hivi wataishije?
Itafika mahali hawa viongozi watashauri kupiga mswaki, Watoto wapelekwe VETAKujua kupika ni life skill.
Yaani tuna viongozi wa ajabu. Hili linaeleza jambo muhimu, kwamba, tatizo si ajira bali wanaopaswa kutafuta ufumbuzi hawana ufumbuzi wala mawazo ya kututoa hapa!Ni jukumu la wazazi nyumbani kuwafunza watoto wao ustadi wa kukabiliana na maisha.
Halafu kupika wala siyo rocket science.
Ugali mtu wa mbeya hayo maigizo tu hahaVery correct nimekutana Na binti mmoja kutoka chuo cha CUOM Mbeya. Ni mzuri mrembo mno sasa. Sasa huwa namuachia funguo mara moja moja nikiwa sipo yeye anakuja kulinda nyumba. Sasa siku hiyo akaja akanikuta akasema anataka kupika ugali dah. Nilishangaa hata kuelezea process za kupika ugali hajui dah nilisikitika sana aise. Hatari huyu yupo chuo kikuu ni mama mtarajiwa. Watoto si watapata malnutrition aise. Hata kupika uji hajui. Taifa hili hata tukikaa litakuja kutawaliwa kabisa 😂
Sasa kama ni mtoto wa fisadi na hajawahi kuijua shida atajulia wapi kupika zaidi ya kuwatumikisha choka mbaya au walalahoi wa nchi hii tena kwa dharau na manyanyaso.Akiwa anazungumza leo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Miaka 50 ya Veta iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni kawaida kuona mtoto amemaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kujipikia chakula chake mwenyewe.
Amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) ina uwezo na jukumu la kubadilisha Tanzania kama jamii itakubaliana watoto kupata stadi fulani kwa ajili ya kuboresha maisha.
View attachment 3278812
Hivi kuchemsha Viazi iwe sweet potato za Mwanza au Irish kunahitaji elimu gani ya VETA..YouTube inatosha kupika chakula chochote kile unachotamani kula.
..ugumu wa kupika sio kwenye mapishi yenyewe, bali kwenye nishati.
..ukishakuwa na jiko la gesi, au umeme, kupika ni kama kumsukuma mlevi.
Cc Nguruvi3