Akiwa anazungumza leo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Miaka 50 ya Veta iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni kawaida kuona mtoto amemaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kujipikia chakula chake mwenyewe.
Amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) ina uwezo na jukumu la kubadilisha Tanzania kama jamii itakubaliana watoto kupata stadi fulani kwa ajili ya kuboresha maisha.
View attachment 3278812