Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Wakuu kwa ufupi kwa wale wenye haraka na muda mchache wa kusoma chapisho zima. Katika hii naibu waziri Godwin Mollel ametembelea ujenzi na kujibizana na Mkuu wa Idara ya Ujenzi (Paul Koroso).

Baada ya majibizano, naibu waziri ametoa amri Paul Karoso aswekwe mahabusu. Na polisi wakamchukua na kumsweka ndani!

Suali langu kwa wadau ana mamlaka naibu waziri wa kuamrisha jeshi la polisi kumkamata mtu na kumueka ndani ? Kanuni na sheria za nchi zikoje ? Nimeshaona issue kama hizi nyingi kiasi cha kuwa zimekuwa zinachengua akili.

chanzo:
 
Kuna ubabe gani kwenye majibu? Huyu naibu waziri kilaza anaamrisha mtu awekwe ndani kwa kosa gani? Jaribu kutumia akili hata kidogo.
kabla ya kusona habari yote nilijua huyu jamaa kamjibu waziri vibaya lakini baada ya kusoma wala sioni kosa lake,kwa sababu yeye amesema yupo tayari kufukuzwa kazi kwa sababu ana uhakika na usahihi wa maelezo aliyotoa,Shida ni kwamba hii serikali ya CCM haipendi watu wanaojiamini,wanataka watu wa ndio mzee
 
Misuse of power ~Baroka
 
Hivi kusema.ukweli ndo utovu wa nidhamu hata kunchinja kichwa kama yohana?Si angeulizwa udhibitisho?
 
Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.

Hii nchi ina vituko kweli kweli
 
Wewe Naibu waziri Mollel unataka wananchi wasiongee na wakuogope wakati unatumia nafasi uliyopewa vibaya na ovyo!. Mamlaka ya kumsweka ndani injia na kuamuru aondolewe kwenye nafasi yake uliyatoa wapi?. Unafahamu kuwa wewe ni mamluki na unaharibu image ya chama Cha mapinduzi?. Haujui kuwa wewe ni msaliti na ndiyo sababu uliwasaliti wananchi waliokuchagua pale ulipojiuzulu ubunge wa chama chako (CHADEMA) kilichokupa nafasi ukashinda Kisha ukakisaliti kwa kujiuzulu without any genuine reasons na ukabebwa sijui kwa mbeleko gani ukajiita mwanaCCM?. Watumishi wa umma kwa muda mrefu wamekuwa ni wahanga wa kudhalilishwa na wanasiasa na ni vema tabia hii mbovu na ya ovyo ikakemewa na kutokomezwa kabisa. Ni vema ukatumie nafasi uliyo nayo vizuri na utambue kuwa cheo ni dhamana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…